Nimeona ni vizuri kuandika ujumbe huu mfupi kutokana na sintofahamu ya watu wengi katika jamii yetu kuhusiana na baadhi ya vyakula kutibu ugonjwa wa COVID-19 .
Kutokana na janga hili watu wengi wamejikuta wakila kundi moja la vyakula kwa madai ya kuuwa virusi vya Corona. Kuna baadhi ambao wanaamini wakitumia juice za limao na tangawizi zitawasaidia kupona ugonjwa wa COVID-19.
Ukweli ni kuwa matunda kama limao na mengine yote yenye uchachu ambayo ni jamii ya machungwa (citrus fruits), mapera, maembe, mananasi, ukwaju, ubuyu na grapes yana kiasi kikubwa cha vitamin C ambayo inasaidia kuimarisha kinga ya mwili.
Utumiaji wa vyakula hivi utakusaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa yote sio COVID -19 pekee. Hivyo basi utumiaji wa vinywaji hivi pekee hautakusaidia kukuponya na ugonjwa huu maana virusi hivi bado havina dawa isipokuwa ni kinga yako ya mwili pekee ndiyo inaweza kukufanya upate nafuu ya haraka endapo utapata maambukizi ya COVID -19.
Jambo la msingi ni kuzingatia kanuni bora za lishe ikiwa ni pamoja na kufanya yafuatayo:
📌Pata mlo kamili wenye mchanganyiko wa makundi muhimu yote ya chakula kama vile wanga kiasi, vyakula vyenye asili ya wanyama na mikunde, mafuta ya mimea, mboga za majani na matunda ya aina mbalimbali kama utaweza kupata bila kusahau maji ya kunywa safi na salama.
📌Fanya mazoezi kuimarisha zaidi afya yako sasa kama utatumia tu hizo chai na juice ukalala siku nzima hatari ya kupata magonjwa ya mfumo wa hewa ni kubwa na kuwa rahisi kushambuliwa na virusi hawa. Jitahidi kufanya mazoezi hata dakika 30 tu kwa siku itakusaidia pia kuimarisha mfumo wako wa hewa na upumuaji.
📌Zuia msongo wa Mawazo. Kwa sasa hofu ni kubwa kulingana na historia ya ugonjwa wenyewe kama ilivyotokea katika mataifa yaliyotangulia kupata janga hili. Kweli hofu ni kubwa lakini ukikaa na kujipa mawazo zaidi unaharibu pia kinga ya mwili wako na kufanya rahisi kwako kushambuliwa na na virusi hawa.
📌Punguza matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara kwa sasa ili kuweza kulinda afya ya moyo wako na mapafu.
📌Kujifukiza na maji ya moto yenye mchanganyiko wa vitu vyenye harufu kama tangawizi, miarobaini, mkaratusi, mchaichai nk itakusaidia kuzuia congestion kwenye airways ( inasafisha mfumo wa hewa) na hata mafua ya kawaida njia hii inasaidia kurahisisha upumuaji. Virusi wanakawaida ya kupotea wenyewe kulingana na nguvu ya kinga yako ya mwili....
📌Jambo la mwisho na la muhimu ni kuchukuwa tahadhari zote tunazoambiwa na wataalamu wa afya.
Maria Samlongo
Afisa Lishe
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Eat healthy stay safe.💞
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment