MAHAKAMA AUSTRALIA YAMWACHIA HURU KARDINALI GEORGE PELL | Tarimo Blog

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MAHAKAMA kuu nchini Australia imeondoa hatia dhidi ya Kardinali  mkongwe wa kanisa katoliki nchini humo George Pell (78) aliyewahi kupatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto na Machi 2019, alihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani lakini uamuzi wa mahakama umemwachilia huru siku ya Jumatatu, Shirika la utangazaji la NBC News patner 7 News la nchini humo limeripoti.

Mahakama kuu ya Australia iligundua kuwa majaji wasiokubaliana walitoa hukumu hiyo na kueleza kuwa walipaswa kuwa na mashtaka kuhusu hatia ya mwombaji kuhusu makosa yote ambayo alihukumiwa na kuamuru hukumu ya Rufaa iingizwe.

Desemba mwaka 2018, Pell alikutwa na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 13, unyanyasaji alioufanya miaka 1990 huko katika kanisa la Melboure, Australia.

Baada ya kutoka Gerezani mapema jumatatu Pell amesema kuwa amepata dhuluma kubwa na kueleza kuwa hamshtaki mshtaki  wake kwa kuwa hataki kuongeza machungu.

Pell ameendela kukana uhalifu huo mbaya ambao umemuweka gerezani kwa miezi 13.

Pell aliyetegemewa kumrithi Papa Francis ametumikia kifungo cha miezi 13 kati ya miaka sita katika gereza la Barwon nje kidogo ya Melbourne.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2