RC Ole Sendeka arejesha ardhi ya wazee iliyotaka kupokwa na wajanja | Tarimo Blog

Na Amiri kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ametoa wiki mbili kwa watu wanne kurejesha ekari mbili za ardhi ya wazee wawili wanaokadiliwa kuwa na miaka zaidi ya 80 zilizouzwa kimakosa, ambayo walipewa zawadi na serikali ya mtaa wa Mji mwema kutokana na kuamsha ari ya taaluma.

Eneo hilo lenye ukubwa ekari 2 linadaiwa kuuzwa na mtu wa jirani wa wazee hao miaka minne iliyopita anaefahamika kwa jina George Angeli ,hatua ambayo imesababisha kuidai haki yao katika vyombo vya sheria.

Ole Sendeka ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea kilio cha wazee hao na kuamua kutembelea eneo lenye mzozo na kudhibitisha uhalali wa umiriki wao ambapo amesema endapo walionunua eneo hilo watahitaji fidia wamfate aliewauzia.

“Msitafute mgogoro na mimi,ninatoa wiki mbili kila mmoja aondoe kilichopo hapa,unataka fidia yako mfuate aliyekuuzia ardhi”alisema Ole Sendeka

Aliongeza kuwa “Kwa ushahidi wa maandishi na kwa maelezo ya walio kuwepo,ardhi hii ilitolewa kwa mr. na mr’s Kalua baada ya wao kustaafu kwenye utumishi kwa nafasi ya ualimu”alisema Ole Sendeka

Mzee Doris Kaluwa na Joseph Kaluwa ambao ni wanafamilia na walimu wastaafu wanasema eneo walilopokwa walipewa na serikali mtaa wa Mjimwema kutokana na mchango wao katika elimu na kudai kwamba uamuzi wa kuliuza eneo hilo haujabarikiwa na wao.

“Sisi hatukumtuma mtu atuuzie viwanja kama tungemtuma tungekuwa tumeenda kwenye ofisi ya kijiji ili waliuziana tu barabarani na sisi tulipata hii ardhi kama zawadi hapa mji mwema”alisema Doris Kaluwa

Wakati wazee hawa wakidai haki yao na serikali kutoa maagizo , Christopher Mwigune ambaye ni moja kati ya watu waliouziwa eneo hilo kimakosa wanasema busara inahitajika kutatua mzozo huo huku mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya mji wa Njombe Lusubila Mwakafuje akidai utaratubu ulivunjwa katika mauziano ya ardhi hiyo.

“Sisi tulikuaja tukanunua kwa mtu lakini inawezekana kweli hiyo changamoto imejitokeza na tayari tumeshawekeza,mimi ombi langu ni hekima inaweza ikatumika”alisema Christopher Mwigune

Kwa upande wake mkuu wa idara ya ardhi wa halmashauri ya mji Njombe, Lusubila Mwakafuje amesema wanunuzi walionunua viwanja kwenye ardhi ya walimu hao wastaafu hawakufuata utaratibu mzuri. “Eneo lolte linapotaka kuuzwa au watu wowote wanaotaka kufanya mauziano ni vema wakapata muongozo kutoka serikali ya mtaa”alisema Lusubila Mwakafuje
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakati akitoa wiki mbili kurejeshwa ardhi ya wazee iliyotaka kupokwa.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe akiwa katika maeneo ya wazee yaliyodaiwa kuuzwa bila kufuata utaratibu na kuirejesha kwa mzee huyo.


 Bi. Doris Kaluwa wakati akitoa taarifa juu ya ardhi yake iliyodaiwa kuuzwa na mmoja wa ndugu yake bila kufuata utaratibu
 Christopher Mwigune mmoja wa wanunuzi wa ardhi hiyo akizungumza taratibu alizotumia kupata ardhi
 Mkuu wa idara ya ardhi  wa halmashauri ya mji Njombe, Lusubila Mwakafuje akitoa ufafanuzi namna ya upataji wa ardhi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2