SHIRIKA la ndege la EMIRATES kuendeleza kuwajali wateja wao kutoa huduma bora | Tarimo Blog


SHIRIKA la ndege la EMIRATES Iimeeleza kuendeleza kujali wateja wao katika utolewaji wa huduma bora hasa katika wakati huu wa mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid -19) vilivyosambaa kote duniani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Mkuu wa Biashara wa Shirika hilo Adnan Kazim imeeleza kuwa janga la Covid -19 halikutarajiwa na amewashukuru wabia wa biashara na wateja wao kwa kuwa wavumilivu, subira na waelewa katika kipindi hiki ambacho sheria zao si rafiki kwa wateja pekee bali pia ni faafu na zinaendana na mahitaji ya kisheria.

Amesema kuwa janga la Covid -19 halikutegemewa na kwa kutambua hilo shirika limetoa nyongeza ya muda wa ziada kwa wateja wao kutumia tiketi zao kwa miaka miwili ambapo nyongeza hiyo itakuwa kwa tiketi zilizokatwa kuanzia Mei 31 hadi Agosti 31 mwaka huu.

"Tunaimani wateja wetu watachagua kusafiri kwa Emirates hapo baadaye na ndio maana tumetoa ofa ya miaka miwili kwa wateja wenye tiketi zao sasa" ameeleza Kazim.

Kuhusiana na wateja wenye vocha za safari amesema kuwa, vocha hiyo itakuwa halali kwa mwaka mmoja tangu ilipotolewa na itatumika kwa huduma yoyote inayotolewa na Emirates.

Amesema kuwa katika wakati huu wa janga la Corona Shirika hilo limeamua kuwaweka wateja wao mbele kupitia sera ya nyongeza  pamoja na fidia kwa tiketi zilizokatwa katika maduka yote ulimwenguni.

Aidha amesema kuwa wametoa ofa kwa  wateja wa Emirates ambao wameathirika juu ya safari yao na hiyo ni pamoja kutunza tiketi zao zilizokatwa kabla ya Mei 31 hadi Agosti 31 mwaka huu  ambazo zitaongezwa muda wa siku 760.

Pia amesema kuwa wateja wenye tiketi za namna hiyo wataheshimiwa na watasafiri wakati wowote watakapoamua kusafiri tena ndani ya miaka miwili kutoka siku ya tiketi ya awali ilipotolewa.

" Emirates haitotoza ada nyingine kama nauli, wateja watatakiwa kuwasiliana na wakala ili kupanga safari zao na tiketi zao zitakubalika katika maeneo yote yanayofikika na Emirates" ameeleza.

Vilevile amesema, wateja waliotunza tiketi zao wanaweza kuomba fidia ikiwa wameshindwa kusafiri na hakutakuwa na adhabu.

Pia Kazim amesema kuwa wateja wanaweza kutembelea tovuti ya shirika hilo kupitia emirates.com ambapo wataweza kupata machaguo yao au kuyachagua pamoja na kupata taarifa na huduma kutoka shirika hilo.

Mwisho.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2