Wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Muhimbili watembelea Kituo cha COVID-19 Hospitali ya Amana | Tarimo Blog

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza jambo wakati alipotembelea  kituo cha watu waliopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha  ugonjwa wa Corona (COVID – 19) cha Amana jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kuona namna ambavyo  madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo watakavyoweza  kutoa huduma kwa wagonjwa hao.

Msimamizi wa kituo cha watu waliopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha  ugonjwa wa Corona (COVID – 19)  Dkt. Stanley Binagi akielezea  jinsi wanavyowahudumia wagonjwa hao wakati wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walipotembelea kituo hicho leo ili kuona namna ambavyo watatoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa hao.
Wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja mara walipomaliza kikao chao na uongozi wa kituo cha watu waliopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha  ugonjwa wa Corona (COVID – 19) cha Amana jijini Dar es Salaam. Wataalamu hao walitembelea kituo hicho kwa ajili ya  kuona namna ambavyo watatoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika kituo hicho. Picha na JKCI


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2