KAMPUNI ya simu za mkononi ya TECNO, imezindua rasmi simu yake mpya CAMON 15 ambayo imesheheni sifa mbalimbali ikiwemo kamera ya nyuma yenye MP64 na mbele MP32 ambayo imewekewa teknolojia kubwa yenye uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo wiki hii jijini Dar es Salaam kupitia mitandao ya kijamii meneja uhusiano wa kampuni hiyo, Eric Mkomoya, alisema simu hiyo itawasaidia sana watu wanaopenda kutumia kamera katika nyanja mbalimbali za maisha wakiwemo wafanyabiashara, wanamitindo, wanaopenda utalii wa kusafiri, wafanyabiashara za mitandaoni, waandishi wa habari pamoja na makundi mengine ya kijamii.
“Simu hii TECNO CAMON 15 ina sifa nyingi sana kubwa na zinazoweza kumridhisha mtumiaji, kamera yake ya nyuma ina MP64 na mbele ni MP32 lakini inatunza sana chaji. Kamera ya simu hii ina uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote hata usiku” Alisema Mkomoya.
Meneja uhusiano wa kampuni ya TECNO Bwana Eric Mkomoya
Aliongeza kuwa TECNO CAMON 15 ni tofauti na simu nyingine kwani hii inapiga picha kwa kuchukua eneo pana zaidi kutokana na kioo chake kikubwa hivyo hata kama mtu anapiga selfie ya zaidi ya mtu mmoja hahitaji kusogeleana kwa karibu hasa kipindi hiki cha janga la maambukizi ya virusi vya corona.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment