Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Bi.Sara Msafiri
Ndg members katika kuongeza udhibiti wa COVID 19 ndani ya wilaya ya Kigamboni serikali inatekeleza mambo yafuatayo:-
1. Kwenye Vivuko:
- kuongeza kivuko kingine, kitaanza kufanya kazi wiki ijayo tarehe 22 April jumatano, Hivyo kutakuwa na jumla ya vivuko vitatu.
- Abiria hawatakusanywa tena kwenye jengo la kusubiria kivuko.
- Kila Abiria atalazimika kunawa mikono kama ilivyo awali.
- Kila abiria atalazimika kuvaa mask muda wote kwenye eneo na ndani ya kivuko, Mask kila mtu kwa gharama zake, zipo za kushona kwa mafundi nguo.
- Serikali inaendelea na jitihada za kupata mashine kubwa za kupulizia watu wanapopita kwenye vivuko, imesha wasiliana na watengenezaji zitafungwa nne kila upande.
- vivuko vitapuliziwa dawa kila baada ya masaa 4.
2. TANROADS wanarekebisha kipande korofi cha barabara cha kuelekea daraja la mwl. Nyerere ili magari yapite na kupunguza msongamano kwenye vivuko. Matengenezo Yatakamilika kabla ya jumatano wiki ijayo.
3. Wananchi wote wa Kigamboni kuanzia umri wa miaka 10 anatakiwa kuvaa mask muda wote anapokuwa nje ya nyumba yake. Hivyo hutapata huduma yeyote iwe dukani, gengeni, gereji, usafiri n.k endapo hutavaa mask. Kila mtu akashone maski. Zoezi hili ni endelevu na utekelezaji wake unaanza ijumaa wiki ijayo. Wajulishe na wageni wenu ili wasije kupata usumbufu waingiapo Kigamboni.
4. Huduma zote za Kijamii na biashara mbalimbali zinaendelea kama kawaida (isipokuwa zile zilizozuiwa na Mhe. Waziri Mkuu na Waziri wa Afya tu) huduma zinazoendelea ni pamoja na hotel, minada, masoko, migahawa, bar ila kila mtu achukue tahadhari. Serikali imeongeza miundombinu kwenye minada Kigamboni kuanzia tarehe 25April.
5. Kila mwenye biashara aweke maji na sabuni yenye dawa au vitakasa mikono. Hakikisha maji yanamwagika na kuingia kwenye mfereji kwa usalama yasisambae na kuhatarisha afya. Team ya afya inapita kufanya ukaguzi.
6. Vijana wenzangu Bodaboda, wacheza karata na bao, wacheza pulltable na kwenye vijiwe vya kahawa. Dada zangu wa saloon na tunaoenda kusuka au kunyoa saloon. Usikubali kuhudumiwa au kupiga story kama hajavaa mask, kumbuka anapokuhudumia anapoongea kunakuwa na chembechembe za mate zinakurukia na utapata maambukizi.
Mwisho nawakumbusha unaponunua bidhaa yeyote kumbuka kudai risiti. Ila kumbuka ukirudishiwa chenchi na risiti yako ukishaweka mfukoni, kumbuka kutakasa mikono yako kwani aliyekuhudumia kama mikono yake ilikuwa na maambukizi basi nawewe mikono yako itakuwa imepata maambukizi. Ukitakasa mikono utakuwa umejikinga Wewe na kuwakinga wengine.
Sara Msafiri
DC Kigamboni.
DC Kigamboni.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment