Kampuni ya TBL Plc imekubaliana kushirikiana na taasisi yaFarm to Market Alliance (FtMA) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) upande wa Tanzania kuwezesha wakulima wadogowadogo wa zao la mtama nchini.Ushirikiano umeanza kwa mradi wa majaribio ambapo TBL Plc imekubali kununua mtama utakaozalishwa na wakulima wadogo wapatao 1,400 kutoka mikoa ya Dodoma na Manyara.Chini ya ushirikiano huo wakulima wa mtama wanawezeshwa kupatiwa mbegu,bima ya mazao,eimu kuhusiana kilimo cha mtama,huduma ya wataalamu wa kilimo,jinsi yak kuongeza mavuno na upanuzi wa masoko.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Plc Philip Redman, amesema mradi huu utafanikisha kuongeza uzalishaji wa mtama nchini Tanzania na wakulima kunufaika kwa kuwa na kipato cha uhakika. Kampuni inanua mtama kutoka kwa wakulima wadogo nchini kwa kushirikiana na FtMA na WFP kuimarisha myoyororo wa thamani na kuboresha maisha ya wakulima wadogo ambao ni wazalishaji wakuu wa zao hilo.
“Tunaamini ushirikiano huu na FtMA and WFP utanufaisha wakulima ambao watawezeshwa kupatiwa mbegu bora, huduma ya kutembelewa na wataalamu wa kilimo kwa ajili ya kuwapatia ushauri hali itakayofankisha ongezeko la uzalishaji wa mtama,” alisema Redman.
Aliongeza kusema, “Tunatarajia kuanza kutumia programu yaununuzi inayojulikana kama BanQu ambayo italeta ufanisi na uwazi katika shughuli zetu za manunuzi.BanQu inawawezesha wakulima kuweka rekodi za mihamala na mahesabu yao kidigitali kama uzalishaji,mauzo,manunuzi ya pembejeo pia inawezesha wakulima kulipwa kupitia simu zao za mkononi.Hii inawewezesha wakulima kuwa na chakula na kuingia katika mfumo rasmi wa kupata huduma za kifedha na kibenki,kuongeza uzalishaji ambapo TBL Plc Kama mnunuzi wa mazao yao itawawezesha kujipatia kipato kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi”
Mwaka uliopita, TBL ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 36.6 kwa ajili ya kununua malighafi kupitia mpango wake wa kununua malighafi ndani “Tunaamini mchango wetu kupitia kununua malighafi zetu ndani unaenda sambamba na jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa Tanzania.” alisema.
“Ukosefu wa soko la uhakika ni moja ya kikwazo ambacho kimekuwa kinarudisha nyuma wakulima katika kuimarisha shughuli zao za kilimo,”alisema Mwakilishi wa WFP nchini,Michael Dunford.Tunapofanya kazi na wakulima wa mtama ili wazalishe zaidi ya matumizi yao ya chakula,tunapaswa kuhakikisha wanunuzi wa mazao yao kibiashara kama TBL wapo ili wanunue hiyo ziada na kunyanyua maisha ya wakulima kiuchumi.”
Mwaka 2018, ABInBev ilijitoa kuwapatia ujuzi, kuwaunganisha na kuwawezesha kifedha wakulima mpaka kufikia mwaka 2025.” Kutokana na mkakati huo, biashara yetu imefanya uwekezaji wenye lengo la kuwainua wakulima wadogo nchini Tanzania kwa kuwaanzishia huduma mbalimbali-Kilimo Uza.
Kutumiwa meseji za simu kuwapatia taarifa mbalimbali kama hali ya hewa, taarifa za masoko, ushauri wa kitaalamu. huduma ya mkopo wa pembejeo, mafunzo khusianana masuala ya fedha na ununuzi wa pembejeo bora na matumizi yake, matokeo ya utafiti wa mbegu bora za mtama unaofaa kuzalishwa nchini, mbinu za kilimo cha kisasa sambamba na kuwasaidia katika kipindi chote cha msimu wa kilimo ili waweze kusimama na kufanya vizuri zaidi”. alisema Redman.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment