Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Trolle Meesle Tanzania Limited ya Mkoani Kigoma inaandaa mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakulima wanachama wa vyama vinane vya ushirika vyenye wanachama 1,850 wanaojishughulisha na kilimo cha michikichi Mkoani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe (Wa Kwanza Kushoto) akipata ufafanuzi kutoka kwa Mwekezaji wa Kampuni Trolle Meesle Tanzania Limited Bw. Abdul Mwilima (mwenye shati la pink) inayomiliki Kiwanda cha kukamua mafuta ya Mawese yatokanayo na zao la michikichi Mkoani Kigoma, Mwambe alitembelea Kiwanda hicho hivi karibuni.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Trolle Meesle Bw. Abdul Mwilima inayotarajia kuwekeza kwenye kiwanda cha kukamua mafuta ya kula yanayotokana na zao la michikichi.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wananchi hao kupata elimu ya kuzalisha michikichi bora itakayotumika kama malighafi kwa kiwanda tarajiwa. Kwa kufanya hivyo pia wananchi wataweza kujiinua kiuchumi mpango unaotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu.
Katika hatua za awali za uendeshaji wa kiwanda, Kampuni ya Trolle Meesle Limited inalenga kununua zao la michikichi (malighafi) kutoka kwa wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika amefafanua Mwilima alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe kwenye ziara ya kikazi Mkoani Kigoma na kupatiwa taarifa ya Maendeleo ya mradi huo wa kiwanda cha kukamua mafuta ya kula yatokanayo na zao la michikichi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Geoffrey Mwambe (Wa Kwanza Kushoto) akipata ufafanuzi kutoka kwa Mratibu wa TIC Kanda ya Magharibi Bw. Innocent Kahwa katika eneo la Kampuni Trolle Meesle Tanzania Limited inayomiliki Kiwanda cha kukamua mafuta ya Mawese yatokanayo na zao la michikichi Mkoani Kigoma, Mwambe alitembelea Kiwanda hicho hivi karibuni.
"Mradi wetu utakuwa na faida nyingi ikiwamo kununua mazao hayo ya wakulima michikichi kama malighafi yatakayopelekea kupata mafuta yenye ubora, wakulima watakuwa na uhakika wa soko, mafuta yatakayozalishwa yana soko kubwa, kiwanda kuwa cha kwanza nchini kuzalisha mafuta ambayo asili ya malighafi ni kutoka nchini, kupunguza 'gap, la mafuta ya kula nchini na fedha nyingi zinazotumika kuagiza mafuta hayo nje ya nchi " alisema Bw.Mwilima.
Akiwa eneo la mradi Bw. Geoffrey Mwambe amewapongeza wawekezaji hao wazawa na kuelezea namna ambavyo mradi wao ni wa tija kwa maslahi ya nchi. Kwa kuzingatia hilo Mkurugenzi amewaambia wawekezaji hao wajitahidi kuhakikisha kwamba mradi unaanza kwa kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula na kuwasihi wawekezaji hao kuzalisha kwa wingi bidhaa hiyo.
"Hivi sasa kama nchi tunahimiza uwekezaji wa aina hii ili kupunguza akisi ya mahitaji halisi ya mafuta ya kula, mafuta tunayozalisha bado hayatoshelezi kwa mahitaji halisi ya nchini kwetu, tunatumia gharama kubwa kuagiza mafuta nje ambayo pia hatuamini sana usalama wake.
Pia amewasihi wawekezaji hao ili kufanya vizuri wahakikishe kwamba uzalishaji wao unajikita katika kutumia mbegu za kisasa zenye uwezo wa kutumia malighafi kidogo lakini mafuta mengi " alisema Mwambe.
Akizungumzia mpango wa mafunzo, Mwambe amesema mpango huo utawanufaisha wakulima wa michikichi kwa kuongeza uzalishaji kwani zao hilo limekuwa na tija ya kiuchumi hususan katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya jitihada za kuhamasisha Uwekezaji katika sekta ya mafuta ya kula ili kupunguza gharama kubwa za uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.
Kiwanda hicho kinachomilikiwa na Kampuni ya Trolle Meesle Limited ya Kigoma kinatarajia kuanza uzalishaji wa mafuta ya mawese mwezi Juni mwaka huu ambapo kitazalisha tani mbili kutoka kwenye michikichi ya kisasa yenye ujazo wa tani tisa.
Mwilima amehitimisha kwa kuishukuru TIC kupitia Kanda ya Magharibi kwa ushirikiano waliompa katika kufanikisha mradi wake ikiwamo cheti cha uwekezaji ambacho kimemsaidia kupata misamaha ya kodi na isiyo ya kikodi katika kipindi cha awali cha utekelezaji wa mradi wake.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment