Wachimbaji Wadogo wa Madini Manyoni Waomba kupatiwa Umeme | Tarimo Blog


Wachimbaji wa Madini wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa madini katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika eneo la Londoni wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 18 Aprili, 2020.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo (kulia)akibadilishana mawazo na mmiliki wa mgodi wa Paulo Msalaba na Washirika, Martin Thomas (kushoto) katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika eneo la Londoni wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 18 Aprili, 2020.
Mmiliki wa mgodi wa Paulo Msalaba na Washirika, Martin Thomas akielezea mafanikio ya mgodi wake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika eneo la Londoni wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 18 Aprili, 2020.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika eneo la  Londoni wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 18 Aprili, 2020.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Tume ya Madini katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika eneo la Londoni wilayani Manyoni mkoani Singida tarehe 18 Aprili, 2020.
………………………………………………………………………….


Na Greyson Mwase, Manyoni

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika eneo la Londoni Wilayani Manyoni
mkoani Singida wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Nishati kuwapatia umeme ili
waweze kuzalisha zaidi madini hivyo kulipa kodi zaidi serikalini.

Wakizungumza katika nyakati tofauti tarehe 18 Aprili, 2020 kwenye ziara ya waandishi
wa habari kwenye machimbo hayo yenye lengo la kuangazia mafanikio ya Sekta ya
Madini katika mkoa wa Singida walisema kuwa wamekuwa wakitumia dizeli katika
kuendesha mitambo ya kuchimba madini hali inayowalazimu kutumia gharama kubwa
na kuongeza kuwa iwapo wangetumia umeme wangeweza kuzalisha zaidi na kulipa
kodi zaidi Serikalini.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo wa madini wengine, mmiliki wa mgodi
wa Paulo Msalaba na Washirika, Martin Thomas alisema kuwa, mbali na maombi ya
umeme, wanaomba kuwezeshwa kupata vifaa vya kisasa vya uchimbaji wa madini ili
waweze kuzalisha zaidi.

“Katika mgodi huu nina wafanyakazi 100 lakini mara baada ya kupata umeme wa
uhakika, nitakuwa nina uwezo wa kuajiri wafanyakazi hadi 300 na kulipa kodi zaidi
Serikalini,” alisema Thomas.

Katika hatua nyingine akielezea hali ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwa
sasa tofauti na awali, Thomas alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Magufuli na Waziri wa Madini, Doto Biteko kwa kuwawezesha
wachimbaji wadogo wa madini nchini kwa kuwapatia maeneo ambapo kwa sasa
uchimbaji wao umekuwa ni rasmi.

Aliendelea kusema kuwa wameshuhudia wachimbaji wadogo wengi nchini
wakihamasishwa kuunda vikundi na kupewa leseni za madini, kuchimba na kuuza
madini yao kupitia masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini katika mikoa yote.

Akielezea manufaa ya masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini Thomas alieleza
manufaa hayo kuwa ni pamoja na madini yao kupata soko la uhakika, kuuza madini
kulingana na bei elekezi zinazotolewa na Serikali, pamoja na usalama wa biashara yao.

Wakati huo huo Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo
alifafanua kuwa maeneo yenye mahitaji ya umeme kwenye machimbo ya madini
yalishaainishwa na kuwasilishwa Wizara ya Nishati kwa ajili ya kupatiwa umeme wa
uhakika.

Katika hatua nyingine, Malembo aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuwa na
subira, wakati wakisubiri kuunganishiwa huduma ya umeme na uchimbaji wao kuwa na
tija.

Aidha mbali na kuwataka wachimbaji hao kuchimba madini kwa kufuata sheria na
kanuni za madini, Malembo aliwataka wachimbaji hao kutumia elimu na miongozo
inayotolewa na wataalam kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya
corona, kujikinga.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2