Chifu wa Ushirikishwaji wa Jamii wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Engelbert Kiondo akitoa mada mpango wa Polisi Kata kama mfumo wa utendaji wa kazi za Polisi kwa sasa wakati wa mkutano wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, mkutano uliowahusisha pia Maafisa Tarafa, Wakaguzi wa Polisi wa Tarafa, watendaji wa Kata pamoja na Askari Polisi wa Kata. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.
Picha na Jeshi la Polisi.
CHIFU wa wa Jamii wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Engelbert Kiondo amesema wazazi wanapaswa kuwa wa kwanza kuwajibishwa kutokana na matendo hasi ya watoto wao ya utoro mashuleni, mimba, utumiaji wa dawa za kulevya, ulevi wa pombe na matendo mengine ambayo ni kinyume na maadili na tamaduni za jamii ya Kitanzania.
Kiondo ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, mkutano uliowahusisha pia Maafisa Tarafa, Wakaguzi wa Polisi wa Tarafa, watendaji wa Kata pamoja na Askari Polisi wa Kata alipopata fursa kutoa elimu kuhusu mpango wa Polisi Kata kama mfumo wa utendaji wa kazi za Polisi kwa sasa.
Ameongeza kuwa, moja kati ya miradi mitano ya mpango wa Polisi Kata ni mradi wa Polisi na watoto, mradi ambao unalitaka Jeshi Polisi kufanya kazi moja kwa moja na wanafunzi, walimu na wazazi ikiwa ni moja ya juhudi ya kujenga nidhamu na maadili ya wanafunzi mashuleni na vyuoni ili kujenga jamii ya watanzania wa kesho wenye madili, nidhamu uzalendo na ari ya kutii sheria bila shuruti.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda amesema elimu waliyopata kutoka Jeshi la Polisi wataifanyia kazi na amewataka watendaji wa kiserikali na wa taasisi zote ndani ya Wilaya anayoisimamia kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana bila na kusukumwa na kuacha kusukumiana majukumu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment