WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUONGOZA MAOMBI YA KITAIFA DHIDI YA JANGA LA CORONA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM | Tarimo Blog


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Viongozi wa madhehebu ya Dini nchini, imeandaa maombi maalum Kitaifa kuiombea Nchi dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayotokana na Virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara, Maombi hayo  yatakayoongozwa na Viongozi Wakuu wa  madhehebu ya Dini nchini, yatafanyika Jumatano tarehe 22 Aprili, 2020 katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar Es Salaam, kuanzia Saa 3.00 Asubuhi ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Taarifa hiyo imebainisha kwamba hatua hii ni utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa viongozi wa Dini na Serikali uliofanyika tarehe 9 Aprili, 2020 Jijini Dar Es Salaam kuwa yafanyike maombi ya kitaifa yanayojumuisha madhehebu yote nchini kuomba dhidi maambukizi ya Corona.

 Aidha, maombi haya ni mwendelezo wa maombi ya siku tatu mfululizo yaliyotangazwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia tarehe 17-19 Aprili, 2020, imesema taarifa hiyo.

 Pia imefafanua kwamba ni viongozi wachache tu ambao watahudhuria maombi haya kuwakilisha wananchi ikiwa ni katika hali ya kuchukua tahadhari ya maambukizi hivyo, wananchi mnasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na kufuatilia maombi haya mkiwa katika maeneo yenu kupitia vyombo mbalimbali vya habari.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2