CHADEMA YAAMUA KUZUIA WABUNGE WAKE KUSHIRIKI VIKAO VYA BUNGE LA BAJETI,KUKAA KARANTINI KWA SIKU 14 KUKABILI CORONA | Tarimo Blog

 Mwandishi Wetu, Michuzi TV

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)kimewataka Wabung wake wote kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti pamoja na kuhudhuria vikao vya  Kamati za Bunge.

Pia Chama hicho kimewataka wabunge wake kujiweka karantini kwa muda usiopungua siku14 kama hatua ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Taarifa ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambayo ameitoa leo Mei 1,2020  kwa vyombo vya habari amesema ni wakati wa kila mmoja wao kuchukua hatua za kijikinga na ugonjwa huo wakati wenye Mamlaka wakisubiri mamlaka kuendelea kuchukua hatua stahiki.

Hata hivyo kabla ya kutoa msimamo wa kuzuia wabunge wao kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti,Mbowe amesema wanasikitika na misiba ya wabunge pamoja na  Watanzania ambayo imekuwa ikitokea na baadhi ya vifo hivyo vinatokana na Corona.

"Kama ambavyo Bunge tumeshuri mara kadaa ,ni dhahiri hatua za ziada zinapaswa kuchukuliwa katika kukabiliana na ugonjwa huo na hiyo itsaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya Corona," amesema Mbowe na kuongeza hivyo Chama chao kimeamua kuanza kuchukua hatua hizo stahiki wa kuzuia wabunge wake kushiriki vikao vya Bunge.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2