DC KIGOMA WASIOVAA BARAKOA KUKAMATWA NA KUCHUKULIWA HATUA KALI | Tarimo Blog

Na Editha Karlo,Kigoma.

MKUU wa wilaya Kigoma Samson Anga ametangaza kuwa watu wote ambao watakutwa hawajavaa barakoa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona watakamatwa na kuchukuliwa hatua.

Anga alisema hayo wakati akieleza tathmini ya agizo la Mkuu wa mkoa Kigoma, Emanuel Maganga  alilolitoa Meo Mosi mwaka huu kutaka watu wote mkoani humo kuanza kuvaa barakoa kuanzia Mei 2 mwaka huu wanapokuwa nje ya makazi yao na kwenye mikusanyiko.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa agizo hilo la Mkuu wa mkoa ni agizo halali la serikali ambapo kila mkazi wa mkoa kigoma anapaswa kulifuata na kwamba kutovaa barakoa ni kukaidi utekelezaji wa agizo hiilo na kwamba hatua kwa wote watakaobainika zitachukuliwa.

Hata hivyo alisema kuwa katika siku ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo idadi kubwa ya wananchi wa wilaya hiyo wameonekana wakiwa wamevaa barakoa na kwamba kadri siku zinavyokwenda jambo hilo litazoeleka na kutekelezwa na watu wote.

Akizungumzia agizo hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya kigoma Ujiji, Mwailwa Pangani alisema kuwa kumekuwa na kujitokeza kwa watu wengi kuvaa barakoa kwenye manispaa hiyo lakini tayari ofisi yake imeshatoa maelekezo kwa watendaji wake kuhakikisha hakuna mtu anayeruhusiwa kupata huduma kama hajavaa barakoa ikiwemo kuingia kwenye masoko ya manispaa hiyo.

Pamoja na hilo Mwiilwa alisema kuwa pia hatua za kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona zinaendelea ikiwemo kuongez matanki makubwa ya kuhifadhia maji kwa ajili ya kunawa mikono kwenye maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu ikiwemo kwenye masoko na vituo vya mabasi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko kuu la Kigoma,Juma Chaurembo alisema kuwa wametoa matangazo kwa wafanyabiashara wote kwenye soko hilo kuvaa barakoa wakati wote lakini pia kutoruhusu mtu yeyote kuingia sokoni akiwa hajavaa barakua.

“Katika siku ya kwanza ya utekelezji wa jambo hili tumeshuhudia watu wengi wamevaa na wale ambao wanakuwa hajwavaa tunawaelewesha na kuwaelekeza barua zinapouzwa, hakuna tatizo la barakoa maana zile zinazoshonwa na mafundi zipo kila mahali na bei yake ni ile ambayo kila mtu anaweza kununua,”Alisema Chaurembo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2