DIWANI KATA YA BOMAMBUZI ATOA MSAADA WA BARAKOA,VITAKASA MIKONO KWA WAFANYABIASHARA | Tarimo Blog

Na Woinde Shizza , KILIMANJARO

DIWANI wa Kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi  Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro Juma Raibu amekabidhi barakoa 100,vitakasa mikono pamoja na ndoo kwa wafanyabiashara wa Soko la Pasua ili kujikinga na virusi vya Corona  ambavyo vinaendelea kutikisa Dunia.

Akizungumza wakati  akikabidhi vifaa hivyo, Diwani huyo amesema kuwa ameamua kutoa vifaa vya kujikinga na Corona kwa wananchi hao ,ili  kuendelea kuchukuwa taathari

Amesemambali na kutoa vifaa hivyo pia ametoa elimu ya kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona 19  kwa wananchi wa Kata ya Bomambuzi pamoja na wafanyabiashara wa masokoni ya Pasua pamoja Mbuyuni huku alibainisha kuwa wataendelea kutoa vifaa vyakujikinga na elimu kwa kila mwananchi.

Aidha amewaomba wananchi hao kufata maelekezo ya wataalamu wa afya na maagizo ya Serikali huku wakizingatia zaidi  kuepuka misongamano isiyo ya  lazima.

Pia Diwani huyo amewaonya wananchi wanaopotosha jamii kuhusu  idadi ya wagonjwa pamoja na  wanafariki kwa virusi vya Corona na kusema kuwa  iwapo atabainika mtu anafanya hivyo hatua Kali zitachukuliwa thidi yake, huku akiliagiza jeshi polisi kuwachukulia hatua kali za kisheriavifaa hivyo .

amesema wamehamasisha jamii juu ya kuweka na kunawa na maji tiririka na sabuni kwenye sehemu zote za biashara nyumbani na maeneo yote yenye mikusanyiko, wametoa elimu kwenye masoko.

Akitoa shukrani kutokana na msaada huo mmoja wa wafanya biashara wa soko la Pasua Gloria Mboya ameema kuwa anashukuru kwa diwani huyo kwa kuendelea kuwajali wananchi wake  kwa kuwapa vifaa vya kujikinga pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kuendelea kuchukuwa tahathari ya ugonjwa huo.

Ameseema kuwa ugonjwa huo upo hivyo ni vyema kila mtanzania  kuendelea kujikinga na kufuata maelezo yanayotolewa na wataalam,huku akikisitiza kuwa iwapo mtu yeyote akijihisi anadalili za ugonjwa huo kuwa maramoja hospital kwa ajili ya kupata  huduma.

 Diwani wa kata ya Bomambuzi na Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uongozi  Manispaa Ya Moshi Juma Raibu akiendelea kuwafundisha wananchi namna ya kuvaa barakoa(picha na Woinde Shizza, Kilimanjaro).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2