GEOFREY JULIUS MCHANGA ANAOMBA MSAADA WAKO WA MATIBABU YA MOYO, MAPAFU NA TEZI YA SHINGO KUOKOA MAISHA YAKE | Tarimo Blog

KILOMBERO, MOROGORO.

KILA Binadamu anapitia mapito aliyoandikiwa na muumba wa Dunia. Kila pito lina njia yake ya kuingia na kutokea.

Tunaamini mpendwa wetu Bwana. GEOFREY JULIUS MCHANGA (Pichani) yupo katika mapito, hakika kwa pamoja tukiungana tutaweza kumsaidia kuwa katika hali yake kama awali.
Kwa sasa  msaada wa haraka unahitaji zaidi kuokoa maisha yake akitakiwa kwenda Dar es Salaam (Muhimbili).

 Anatakiwa kufanyiwa vipimo zaidi na upasuaji wa matatizo yake yanayomkabili ya maradhi ya ukubwa wa Moyo, mapafu kuwa na ukungu na tezi shingoni (tezi ya shingo).

Matibabu hayo yanahitajika kufanyiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Gharama za awali za kuanzia matibabu yake ni shilingi Milioni moja na Laki tano (1,500000 ).

Na kiasi cha chini cha shilingi Laki tano kwa ajili ya gharama za matumizi ya usafiri, malazi na chakula yeye na msimamizi wake.

Hivyo tunakuja kwenu kuomba chochote ilikufanikisha kiasi cha shilingi Milioni 2.

Kwa sasa jukumu hilo linasimamiwa na vijana aliomaliza nao kidato cha nne 2013 wakiongozwa na Sweatbert P James ama MC Zakayo Mtozaushuru wa Mtozaushuru Entertainment.

"Sisi vijana kwa pamoja  ambao tulisoma nae 2013 tunakuja mbele yako    kuomba msaada wa hali na Mali kwa niaba ya ndugu yetu mpendwa, Bwana Geofrey.

Kwa mujibu wa Madaktari wa awali alipokuwa akipata tiba huku Kilombero wamependekeza apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi ya kina." Alisema Sweatbert Jamese 'Lazaro Mtozaushuru'.

Kwa mawasiliano zaidi/kutuma msaada wako tumia namba ya  MC ZAKAYO MTOZAUSHURU jina la usajili litatokea  SWEATBERT P JAMES:
 +255 688 523 165.

Namba ya Geoffrey  (Muhitaji wa matibabu):
+255677671984.

AU;
Msaada wa kuweza kupata Daktari atakayesaidia kumpatia matibabu ya haraka.

"Lengo letu sote  ni kuhakikisha ndugu yetu ana rejea katika hali yake ya kawaida. Yote yana wezekana kwa msaada wa Mwenyezi Mungu".

Hadi sasa Geoffrey  ameshapata barua ya rufaa kupelekwa Muhimbili,  lakini hatuna hata ya kuanzia.

"Tunamuangaikia fedha za chakula na mahitaji mengine hali yetu ni duni sana, hivyo tunazidi kuwaangukia Wadau, ndgu, marafiki na jamaa popote pale mlipo".

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2