HUYU NDIE RAIS WA KARNE JPM | Tarimo Blog

Leo nimemsikiliza kwa Makini san Rais wetu Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akimuapisha waziri wa katiba na Sheria Mhe Mwigullu Madelu Nchemba na haya ndio mananeo yaliyogusa moyo wangu

-JPM yuko tayari kutuma ndege kwenda Madagascar kuleta dawa inayotajwa kutibu virusi vya korona, hapa anamanisha yuko tayari kufanya chochote chema kwa wananchi wake

- JPM ameonyesha kusikitishwa na jinsi watu wanaofariki na korona wanavyoshughulikiwa akitolea mfano tukio la Marehemu Dc Evod Mmanda ameshangaa kwanini hakupelekwa kwao Moshi, hapa ameonyesha mfano huu kuonyesha kukerwa na hata wananchi wengine wanavyotendewa katika mchakato wa kusitiri watu wao

- JPM amesikitishwa na baadhi ya viongozi wa dini ambao wameanza kuogopa korona kiasi cha kuweka vitabu vyao vya dini uvunguni na kuhofia maisha yao, hii ni aibu kwao na sisi tunaendelea kujifunza kutokana na matendo yao, hapa anaonyesha kukerwa na baadhi ya watu kurudi nyuma katika mapambano haya haswa wale ambao tunawategemea watakuwa mstari mbele kwetu, sasa najua wako baadho ya viongozi wa dini maisha yao ni bora kuliko ya wanaowaongoza

- JPM ameonyesha dhahiri udhaifu wa baadhi ya wataalamu katika maabara kwa kushindwa kutoa majibu sahihi ya sampuli wanazopelekewa na badala yake amegundua mpaka papai na mbuzi wana korona , hapa anamanisha sio kila mtu anaefariki anafariki na korona na sio kila sampuli inayopimwa ni kweli korona

Mhe Rais Magufuli amesema maneno mengi mazito, yenye ukali ndani yake, huyu ndie Rais tunaemtaka anaeweza kusimam mstari wa mbele katika kuwaongoza wananchi pasipo hofu, Mhe Magufuli amesimama katika nafasi yake kama amiri jeshi mkuu, amesimama katika nafasi yake kama kiongozi mkuu wa dini, amesimama katika nafasi yake kama baba wa familia na amesimama katika mstari wa mbele wa mapambano ya vita dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya korona COVID - 19 .

Huyu ndie Rais ambae Mungu ametupa watanzania, leo ameniongeza ujasiri na moyo wa kuendelea kupambana na ugonjwa huu uku nikiwa katika mstari wa mbele wa kuongoza wananchi wa Arumeru Kwa matendo.

Vitabu vya dini vinatuambia tutawatambua kwa matendo yao, na sio maneno wala kelele zao

*Baba ameshasema tuchape kazi *

*Jerry Cornel Muro *
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
03/05/2020
[1:05 PM, 5/3/2020] Michuzi Airtel: Rusha

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2