Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NI miaka 102 sasa tangu Thomas Carter mwanafunzi wa Georgia aliyekuwa akichukua shahada ya uhandisi kuchukua picha iliyowaonesha mashabiki wakiwa wanatazama mpira katika kipindi cha mlipuko wa homa kali ya mafua (Spanish Flu) mwaka 1918.
Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi wakati huu ambao shughuli mbalimbali zikirejea duniani ikiwemo michezo na hiyo ni mara baada upepo mkali wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19) kupiga ulimwenguni kote na kusababisha vifo kwa maelfu ya watu.
Picha hiyo inaonesha mashabiki waliovaa barakoa na gloves wakiwa wamekaa kwa kuachiana nafasi wakifuatilia mechi ya nyumbani ya timu ya Georgia Tech kwenye ligi, maarufu "College League." mwaka 1918.
Wakati huo michezo iliendelea huku tahadhari ya ugonjwa huo zikichukuliwa na hiyo ni kwa tamko la Rais wa Marekani wa wakati huo Woodrow Wilson kupitia barua ambayo iliwekwa hadharani 1919.
Mwaka huo wakati wa mlipuko wa homa kali ya mafua (Spanish flu) ilisababisha vifo takribani 642, 000 ndani ya Marekani.
Ni mwisho wa mwezi Mei 2020, baada shughuli nyingi duniani kusimama kwa muda mrefu kutokana na mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona, na sasa shughuli mbalimbali ikiwemo michezo zimeanza kurejea, nchini Tanzania Rais Magufuli tayari ameruhusu kuendelea kwa shughuli za michezo ambayo huwaweka watu pamoja na tayari timu zameanza kujiandaa kwa ajili ya mechi zitakazochezwa nyumbani na ugenini na kimataifa ligi kuu ya Uingereza milango imefunguliwa na Juni 17 michuano hiyo itaendelea huku tahadhari zikiendelea kuchukuliwa zaidi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment