Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirika la ndege la Precision Air wamezindua safari za ndege ya mizigo kutokea Tanzania na kuelekea Hahaya katika Visiwa vya Comoros wakipeleka bidhaa mbalimbali.
Safari hizo zimeanza rasmi siku ya Jumamosi kutokana na mabadiliko katika soko na nchi nyingi kufunga mipaka yao.
Akitoa taarifa hiyo, Meneja Masoko na Mawasiliano amesema wamebadilisha moja ya ndege zao aina ya ATR72-500 kuwa ndege ya mizigo, na safari ya kwanza ilikuwa ni siku ya Jumamosi.
Amesema, kutokana na mabadiliko katika soko safari yao ya kwanza ya mizigo kuelekea Hahaya waliweza kusafirisha madawa pamoja na mbogamboga.
Mremi ameeleza kuwa Kupitia safari hiyo ya kwanza pia wamezindua rasmi safari za mizigo ambapo zitakuwa zikifanyika kila Jumatano kuelekea Hahaya.
Mremi amesema, ndege hyo ya ATR72-500 ina uwezo wa kubeba tani 5.5 kwa wakati mmoja na itapeleka mahitaji muhimu kila wiki.
Aidha, safari za ndani na kikanda zitaendelea kulingana na mahitaji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment