Moja ya jengo jipya na la kisasa la Shule ya Sekondari ya Wasichana Jokate Girls iliyopo Kata ya Kibuta wilayani Kisarawe mkoani Pwani ambayo linavyoonekana.Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemen Jafo amefanya ziara ya kutembelea shule hiyo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wake.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo akizungumza jana baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya bweni ya wasichana inayojengwa Kijiji cha Mhaga katika Kata ya Kibuta wilayani Kisarawe.Waziri Jafo ameagiza shule hiyo ipewe jina la Jokate Girls Sekondari kama sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye ndiyo ameijenga.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana inayojengwa Kijiji cha Mhaga ,Kata ya Kibuta wilayani humo.Majengo ya shule hiyo ni ya kisasa zaidi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo(kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(kulia) pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali wa wilaya hiyo wakielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa moja ya jengo la shule ya bweni ya wasichana.Waziri Jafo ameagiza shule hiyo iitwe Jokate Girls Sekondari.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe(katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mussa Gama wakiwa katika maombi wakati ikisomwa dua kwa ajili ya kuwambea viongozi hao kwa Mungu kutokana na jitihada ambazo wanazifanya za kuwatumikia wananchi.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Tella Mwampamba (aliyesimama) akitoa utambulisho wa viongozi wa wilaya hiyo kwa Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana ya Jokate Girls Sekondari.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo akipata maelezo kuhusu ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana inayoengwa kijiji cha Mhaga katika Kata ya Kibuta wilayani Kisarawe baada ya kutembelea shule hiyo kangalia maendeleo ya ujenzi wake ambapo ameridhishwa a ubora wa majengo ya kisasa yaliyojengwa na kuagiza iitwe Jokate Girls Sekondari
Baadhi ya magodoro ambayo yatatumiwa wanafunzi ambao watapata nafasi ya kujiunga na shule ya bweni ya wasichana inayojengwa katika kata ya Kibuta wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo ameridhiwa na ubora wa majengo ya shule hiyo ambayo ni ya kisasa.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo(katikati aliyevaa gauni) akiwa na wana kamati wa kujitolea ambao wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana ambayo Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo ameagiza iitwe Jokate Girls Sekondari.
Muonekano wa majengo pamoja na mandhari nzuri ya shule ya bweni ya wasichana ambayo inajengwa katika Kijiji cha Mhaga ,kata ya Kibuta wilayani Kisarawe. Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemen Jafo ameridhishwa na ujenzi wa shule hiyo ya kisasa ndani ya wilaya hiyo ambapo ameagiza ipewe jina la Jokate Girls Sekondari.
======= ======== =========
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KUTOKA moyoni nimefurahi sana sana!Hiyo ni kauli ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo ambayo ameitoa baada ya kuridhishwa kwa kiwango kikubwa na ujenzi wa Shule ya bweni ya wasichana ambayo imejengwa katika Kijiji ya Mhaga ,Kata ya Kibuta wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Waziri Jafo tayari ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Ofisa Elimu Wilaya kuanza mchakato wa kusajili jina la shule hiyo ambapo ameamuru iitwe Jokate Girls School kama sehemu ya kutambua mchango na jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye amefanikisha kujengwa kwa shule hiyo ya kisasa wilayani humo.
"Shule hii kwasababu DC wangu ulibeba maono ,shule hii nataka niite Jokate. Huo ndio uamuzi wangu na sababu kubwa DC Jokate aliamua ufanya kazi na kubeba maono yangu mimi, shule nzuri sana kama ulivyo mweyewe na Mungu akubariki sana.Tunataka shule hii iwe bora sana hapa nchini,"amesema Waziri Jafo huku akimwagia Sifa Jokate kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na kwamba Jokate ni moja ya wakuu wa Wilaya bora nchini.
Akifafanua zaidi Waziri Jafo amesema nguvu kubwa ya utendaji wa Jokate katika shule hiyo ndio umemfanya kuamua iitwe jina lake na amesema kwa Kisarawe kuna kila sababu ya kutambua moyo wa uzalendo na upendo wa Mkuu huyo wa Wilaya kwa kumpa heshima hiyo.
"Narudia tena kueleza hapa hadharani DC Jokate anafanya kazi sana tena kwa vitendo , ni mbunifu na anabeba maono yenye uzalendo mkubwa kwa nchi yake.Katika Wilaya ya Kisarawe wamepita viongozi wengi sana lakini sijawahi kuona kiongozi mchapa kazi kama Jokate na kutoka moyoni namtakia heri katika utendaji wake na Mungu amsimamie apande zaidi ya hapa alipokuwa,"amesisitiza.
Waziri Jafo ametumia nafasi hiyo kuifichua siri ya uchapakazi wa Jokate ndani ya Wilaya ya Kisarawe kwani baada ya Rais Dk.John Magufuli kumteua kwenye nafasi hiyo alimuita ofisini kwake na kisha kumueleza kuhusu Kisarawe na hakika ametenda haki kwani yote ambayo amemueleza ameyafanyia kazi kwa asilimia 100 na wananchi wa wilaya hiyo ni mashahidi.
"Wananchi wa Kisarawe naomba leo niwaambie baada ya kufanya mazungumzo na Jokate baada ya kuteuliwa na Rais, nilimueleza mambo mengi na leo hii amenithibitishia kwa vitendo niliyomueleza yalimuingia na ameyabeba maono yangu.Kisarawe tumepata bahati kubwa ya kuwa na Jokate pamoja na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi na Katibu Tawala ambao wote ni vijana na wazalendo kwa nchi yetu,"amesema Waziri Jafo.
Kwa upande wake Jokate akizugumza baada ya Waziri Jafo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo , amesema anawashukuru watu wote ambao wameshiriki kila hatua kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unafanyika na hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaomba waendelee na moyo wa uzalendo na kuipenda nchi yao.
"Tumefika hapa leo na shule yetu inaonekana ilivyo kwasababu watu waliamua kubeba maono yetu ya Tokomeza Zero Kisarawe kwa moyo mmoja, wamejitoa kwa michango na mawazo, nawashukuru wote,"amesema Jokate na kusisitiza kuwa Kisarawe wao wataendelea kuchapa kazi kama ambavyo Rais Dk.Magufuli amekuwa akisisitiza siku zote.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment