Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
ANAFAHAMIKA kwa jina la Anorld Alois Schwarzenegger "Styrian Oak" au "Australian Oak" amezaliwa Julai 30,1947 akiwa na uraia wa Australia na Marekani kilichompa umaarufu zaidi ni pamoja na uigizaji, siasa akihudumu nafasi ya gavana wa 38 katika jimbo la Colifornia kutoka mwaka 2003 hadi 2011, mwanamazingira na pia ni mtengenezaji wa filamu, mtunzi, mfanyabiashara na mtaalamu wa kujenga mwili kwa mazoezi.
Anorld ni kijana na askari (Gudtav Schwarzenegger) ambaye alipigana katika vita ya pili ya dunia na amenukuliwa akieleza namna baba yao alivyowaweka katika mstari hasa pale wakifanya jambo baya ikiwemo kufanya ukaidi kwa wazazi, na ameeleza alikuwa karibu zaidi na mama yake kipenzi (Aurelia.)
Akiwa shule Anorld aliripotiwa kuwa na uwezo wa wastani darasani ila alikuwa na tabia njema iliyowavuta wengi, alinukuliwa akisema fedha kwao haikuwa tatizo sana na amewahi kueleza akiwa mdogo alishuhudia familia yake ikinunua friji, amefanikiwa kupata shahada katika chuo kikuu cha Wisconin.
Alipofikisha miaka 14 alichagua fani ya kujenga mwili kwa mazoezi dhidi ya soka na akaanza kutembelea viwanja mbalimbali vya mazoezi ambako alikutana na wacheza filamu na ndoto yake kuigiza ikatimia mwaka 1970 kwa kuuigiza filamu yake ya kwanza ya "Hercules in New York" huku movie zake zilizopendwa zaidi ni pamoja na Terminator, Predator na Expendables.
Akiwa na miaka 15 tuu Schwarzenegger alianza kutengeneza mwili kwa mazoezi na alipofikisha miaka 20 alishinda shindano la Mr. Universe na baadaye kushinda mara saba zaidi shindano la Mr. Olympia huku akitajwa kuwa body builder wa miaka yote duniani.
Oktoba 7, 2003 Anorld alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuliwakilisha jimbo la Colifornia kwa tiketi ya chama cha Republican na alihudumu hadi mwaka 2011 na uongozi wake unaelezwa kuwa wa pekee katika jimbo hilo hasa kwa kutekeleza miradi mingi hasa katika sekta za maji, mazingira na miundombinu na alipomaliza muhula wake wa mwisho alirejea katika uigizaji.
Anorld amekuwa akitumia nguvu zake pamoja na kipato binafsi katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu na kwa kutambua mchango wake katika uongozi Anorld amepata tuzo nyingi zikiwemo za "National Leadership Award" na "Renewable Energy Leader of the Decade."
Anorld na mkewe Maria Shriver wamebarikiwa watoto watano.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment