Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli akitoa ripoti ya kurejea shuleni kwa wanafunzi wa kidato cha sita.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Gerald Mweli amesema asilimia 90 ya wanafunzi wa kidato cha sita wameripoti shuleni katika halmashauri zote nchini.
Mweli amesema mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kuwapo kwa maambuziki ya ugonjwa wa Corona kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioripoti shuleni.
Akitoa tathimini ya uripotiji wa wanafunzi shule ambao walitakiwa kuanza masomo Juni 1 mwaka huu, Mweli amesema wanafunzi hao wameanza masomo yao majuzi na kuwa leo wataanza kufanya mitihani ya majaribio ili kufanya tathimini ya maeneo ambayo wanafunzi yanawasumbua.
Mweli amesema mpaka sasa hakuna taarifa ya kuwapo kwa mwanafunzi mwenye dalili za kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
“ Napenda niwatoe hofu wazazi kuwa watoto wana afya njema na kuanzia jana na leo (juzi na jana) hatuna tukio au taarifa ya kuwapo mwanafunzi yeyote mwenye dalilia za kuwa ameambukizwa ugonjwa wa Corona.
Tumejipanga kuwa na maji ya kutosha, sabuni za kutosha katika shule zetu na kuzingatia suala la umbali wa mwanafunzi mmoja na mwingine ili kuwafanya wanafunzi wetu kuwa salama," Amesema Mweli.
Amesema katika shule zote kumekuwapo na maandalizi mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwa shule zote zimezingatia mwongozo uliotolewa na wizara ya afya juu ya kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.
" Nimategemeo yetu kuwa ndani ya wiki mbili kutoka sasa wale wanafunzi ambao watakuwa wamefanya mitihani ya majaribio watakuwa wamesahihishiwa na kubaini maeneyo yenye upungufu ili kufanyia kazi kabla ya mitihani ya mwisho, " Amesema Mweli.
Amesema Tamisemi imeandaa program maalumu ya kuhakikisha topiki ambapo zimewatatizia wanafunzi zinafanyiwa marejeo.
“ Nitoe wito kwa walimu na wakuu wa shule kuwa mipango tuliojiwekea na hali inavyokwenda sasa tuhakikishe tunasimamia na tunakuwa karibu na watoto na kuzungumza nao mara kwa mara na kuzidi kuwapa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona," Amesisitiza Mweli.
Aidha amewataka walimu, wakuu wa shule na mameneja wa shule binafasi kuhakikisha wanatekeleza katazo la kuwataka wanafunzi kwenda shule na tangawizi, malimao.
Aidha, Mweli alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamaia kwa karibu shule zilizo maeneleo yao ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama mpaka hapo watakapomaliza mitihani yao ya kidato cha sita.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment