Zaidi ya milioni mia nne ishirini na saba zimetumika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule,barabara na madaraja kwa kipindi cha miaka mitano katika kata ya Udonja wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya udonja Hapnes Bomba wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitano, ambapo amesema fedha hizo zimetolewa na serikali,mbunge wa jimbo la Wanging'ombe na wadau wa maendeleo wakiwemo wananchi.
Aidha katika kipindi cha miaka mitano diwani huyo amesema amefanikiwa kuviwezesha vikundi 19 vya wanawake,vijana na walemavu kupata mkopo wa milioni 31 usio na riba kutoka halmashauri ya wilaya hiyo kupitia idara ya maendeleo ya jamii.
“Tumefanikiwa kulima barabara zinaounganisha kata ya Ilembula na kata Usuka,barabara ya Ngamanga kata ya Utengule,vikundi 19 vya wanawake vijana na walemavu vimekopeshwa mkopo bila riba kutoka halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkopo wenye thamani ya milioni 31”alisema Hapnes Bomba
Nae Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Udonja Isaka Dononda amesema kuwa kile ambacho kimefanywa na diwani huyo ndicho ambacho walimuagiza.
“Nina uhakikia yote aliyoyazungumza ndivyo tulivyomtuma na alizungumza kwenye Ilani yetu ya mwaka 2015 lakini amefanaya na amepitiliza hata kwenye Lengo ambalo aliahidi kufanya”alisema Isaka Dononda
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa kata hiyo ya Udonja wamesema kuwa awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa miundombinu ya barabara lakini kwa sasa inapitika.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment