Ndege ya mizigo kuimarisha usafirishaji samaki nje ya nchi | Tarimo Blog


Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mipango ya Serikali kununua ndege ya mizigo utaimarisha usafirishaji wa minofu ya samaki moja kwa moja kwenda nje ya nchi kutokea uwanja wa ndege wa Mwanza.

Waziri Kamwelwe ameyasema hayo Jumatatu Juni Mosi 2020 jijini Mwanza wakati akifungua mkutano wa kupokea mikakati ya pamoja kuondoa vikwazo na kufanikisha biashara ya usafirishaji minofu ya samaki kwenda nje ya nchi hususani mataifa ya Ulaya ambako kumekuwa na soko la uhakika.

Kikao hicho kimewajumuisha pia Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mifugo na Uvuvi, Viwanda na Biashara pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katika) akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2