TAKUKURU DODOMA YAWAONYA WATAKAOTOA NA KUPOKEA RUSHWA UCHAGUZI CHAMA CHA WALIMU | Tarimo Blog

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthnes Kibwengo akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.

Charles James, Michuzi TV
ZIKIWA zimebaki siku mbili kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Viongozi wa kitaifa wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Dodoma imetoa onyo kwa wale wote watakaotoa na kupokea Rushwa.

Uchaguzi huo wa CWT utafanyika Juni 5 jijini Dodoma ambapo utachagua Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na viongozi wa makundi maalum yakiwemo Walemavu, Vijana na Wanawake.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthnes Kibwengo amewataka wajumbe na wagombea wote wa Chama hicho kufuata utaratibu wa CWT na sheria za nchi ili wajiepushe na vitendo vya rushwa.

Amesema Takukuru Dodoma haitomvumilia mtu yeyote ambaye atajaribu kuchukua au kutoa rushwa kwenye uchaguzi huo.

" Niwasihi sana ndugu zetu Walimu tunafahamu wanakuja kwenye mkutano wao mkubwa kabisa ambao utafanyika hapa kwetu Dodoma, rai yangu kwa wote ni kufuata utaratibu wa chama chao na sheria za Nchi yetu.

Yeyote atakayevunja kifungu cha 15 cha sheria kwa kuomba ama kupokea rushwa anatakiwa afahamu kwamba Takukuru Dodoma hatutomuacha salama, lengo letu ni kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa utulivu bila kuwepo mazingira yoyote ya rushwa," Amesema Kibwengo.

 Katika hatua nyingine Kibwengo amesema Takukuru Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kurejesha kwa wananchi 13 mashamba yenye ekari 30 na nyumba mbili kutoka kwa mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Nelson Ndalu.

Wananchi hao wa Kijiji cha Makole wilayani Kongwa walipoteza mashamba na nyumba zao kwa Ndalu ambaye amekua akiwakopesha bila kufuata utaratibu kwa kutoa mikopo kandamizi yenye riba kali inayowaumiza watu.

" Tumefanikiwa pia kurudisha Mali za wananchi wetu ambazo zilikua zimechukuliwa na Bw Ndalu. Niwaombe wananchi wa Dodoma kufuata utaratibu wa mikopo na pale wanapoona kuna vitendo vya kudhulumiwa wawasiliane na Takukuru haraka, " Amesem Kibwengo

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2