Na Woinde Shizza , ARUSHA
BARAZA la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira Kanda ya kaskazini (NEMC) limewataka wananchi kutunza mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja Meneja wa kanda ya kaskazini Lewis Nzali alisema uharibifu wa mazingira unachangia kwa kiasi kikubwa kupoteza kwa baadhi ya viumbe hai maarufu kama bionuai pamoja na hali ya jangwa na ukame.
Alisema kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali za kimazingira ambapo alitaja baadhi ya changamoto hizo ni uharibifu wa Aridhi ,ufyekaji na uharibu wa misitu,uharibifu wa vyanzo vya maji,uharibifu wa makazi ya viumbe wa majini pamoja na upotevu wa bioanuai.
Aidha Nzali alisema maadhimisho ya mazingira duniani hufanyika juni kila mwaka ambapo kilele kinatarajiwa kufanyika June tano mwaka huu na kilele hicho kulikuwa kifanyike mkoani Lindi lakini
Alibainisha Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali ikiwamo uharibifu wa Ardhi.
Akieleza zaidi alisema Arusha inaongoza kwa kuwa na viwanda vingi jambo ambalo kwa baadhi ya Viwanda pamoja na kuwa na vyeti vya tathmini ya uharibifu bado makosa yamekuwa yakifanyika na kutokana na kutofuata sheria zilizowekwa katika Vyeti vya Ithibati.
Hata hivyo amewasisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira pamoja na kuhakikisha wanaotesha miti ya asili ili kupunguza ukame unaoweza kusababishwa na upotevu wa maji ardhini.
Alisema Kuhifadhi mazingira sio jukumu la serikali peke yake Bali ni la kila mtu kwa nafasi yake ,hivyo wawekezaji na wananchi kujitahidi kutimiza wajibu na kutunza mazingira yetu kwa faida ya afya zetu na viumbe wengine ,kwa faida ya kizazi Cha Sasa na kijacho.
Alibainisha Kuhifadhi mazingira ni wajibu wa kila mtu aishiye Tanzania,hivyo ni muhimu kwa kila mtu kushiriki katika kutunza mazingira kwa kushiriki Kuhifadhi mazingira,na kuepuka au kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na uharibu wa mazingira katika ardhi,misitu,vyanzo vya maji na nchi kavu vinavyoweza kusababisha upotevu was bioanuai pamoja na uchavufuzi wa hewa kutokana na viwanda.
Maadhimisho ya Mazingira kitaifa yalikuwa yafanyike Mkoani Lindi lakini kutokana na kuwepo kwa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona haitafanyika badalada yake elimu itatolewa kwanjia ya vyombo mbalimbali vya habari ,mitandao ya kijamii , midahalo mbalimbali kupitia njia ya video pia wameandaa mashindano ya uandika insha mbalimbali zinazo husu mazingira .
Meneja wa baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira Kanda ya kaskazini (NEMC) Lewis Nzali akiongea na waandishi wa habari ofisini kwakwe Jana zilizopo Ndani ya jiji la Arusha juu ya wiki ya mazingira ambayo kilele chake kinafanyika Juni tano mwaka huu ambapo aliwataka wananchi kutunza mazingira ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi(picha na Woinde Shizza).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment