Na Janeth Raphael ,Michuzi TV
JIMBO la Kibamba jijini Dar es Salaam ni moja kati ya majimbo yaliyokuwa na ushindani mkubwa kwenye mchakato wa kura za maoni kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) waliojitosa kuomba ridhaa ya kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama hicho.
Ushindani ulikuwa mkubwa,tena mkubwa haswaaa.Zipo sababu nyingi za kuufanya mchakato huo kuwa na ushindani na mojawapo ni idadi ya waliojitokeza na sifa za kila mgombea.
Hata hivyo ushindani mkubwa ilikuwa kati ya Issa Jumanne Mtemvu ambaye ndiye aliyeshinda kwa kupata kura 83 dhidi ya Vicky Kamata aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 49.
Wawili hao walikuwa kwenye ushindani kwasababu wote ni wazoefu katika medani za kisiasa. Tukianza na Vicky Kamata ni mwanamama ambaye amedumu jimboni kwa vipindi viwili mfululizo akitumikia Mkoa wa Geita.Alikuwa Mbunge wa Viti maalum.
Historia ya Vicky Kamata kwenye siasa iko vizuri na amekuwa na mchango mkubwa kwa Chama chake, wananchi wa Mkoa wa Geita na Watanzania.Amefanya kazi nzuri.Kwa mashabiki wa muziki wanakumbuka kibao cha Wanawake na Maendeleo.Ni kibao ambacho kimeimbwa na mwanamama huyo aliyekuwa kwenye mikono ya CCM.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Issa Jumanne Mtemvu yeye, amewania ubunge kwa vipindi viwili mfululizo na kukosa na ndipo amejitokeza tena kuwania na hatimaye kura za maoni ndani ya CCM zimetosha.Mtemvu anazijua siasa vizuri.
Baada ya matokeo kutangazwa Michuzi Tv kama kawaida yake ya kuhakikisha watanzania wanapata kila kinachoendelea kwenye mchakato iliamua kufanya mahojiano ya ana kwa ana na Vicky Kamata ambapo amesema amefurahishwa na ushindani na amempongeza aliyeshinda kwenye kura za maoni.
"Kwa kweli nimefurahishwa na mchakato huu wa awali hii ni hatua muhimu sana katika maisha yangu kisiasa baada ya kuhudumu kwa kipindi Cha miaka 10 mfululizo kwa kuteuliwa viti maalumu.
"Niliamua kujipima ni kwa jinsi gani nakubalika majimboni? Kwa kweli nimefurahi ' Am Super Women'.Nimejiona naweza nawaahidi wana Kibamba na huu ni mwanzo tu mazuri yanakuja, hizi ni kura za maoni tusubiri Kamati Kuu wataamua,"amesema Kamata
Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wajumbe wote waliompigia kura na pia amepongeza viongozi waliosimamia mchakato huo mzima ulioanza sa tano asubuhi mpaka sa nne usiki alipopatikana mshindi.
Issa Jumanne Mtemvu (kushoto) akihesabu kura zake ambaye ndiye aliyeshinda kwa kupata kura 83 katika jimbo la Kibamba wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam ,Vicky Kamata alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 49.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Vicky Kamata (kushoto) akihesabu kura zake ambaye ndiye aliyeshika nafasi ya pili kwa kura 49 katika jimbo la Kibamba wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wajumbe Halali wa kikao wakifuatilia matukio mbalimbali katika (Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Sehemu ya wagombea.
Wajumbe Halali wa kikao wakipiga kura
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment