CHAMA CHA NRA CHACHAGUA MGOMBEA WAKE WA URAIS BARA NA ZANZIBAR | Tarimo Blog

 Mgombea wa nafasi ya Urais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leopold Mahona (kushoto) akiwa na mgombea mwenza Khamis Ali Hassan (Katikati) na Mgombea wa Urais wa Zanzibar Khamis F Mgau wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho wa Kumchagua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Hassan Almas akitangaza matokeo ya Uchaguzi  wa  Mkutano Mkuu wa Chama hicho  wa kumchagua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais Zanzibar.
 Viongozi wa tume ya uchaguzi wa Chama cha NRA wakihesabu kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho  wa kumchagua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha NRA Simai Abdulla akizungumza na wanachama wa Chama cha NRA wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho  wa kumchagua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais Zanzibar.

Msajili Msaidizi idara ya usajili wa vyama, Sixty Nyahoza akizungumza na wanachama wa Chama cha NRA wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho  wa kumchagua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais Zanzibar.

 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha NRA wa  kumchagua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais Zanzibar.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Chama cha Siasa cha National Reconstruction Alliance (NRA) kimempitisha  Leopold Mahona kuwa mgombea wa Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

NRA wamefanya mkutano wao mkuu leo Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Mikoani 16 Tanzania Bara na 4 visiwani Zanzibar.

Mahona  amepata kura 61 sawa na aslimia 57, akiwashinda Mwanaenzi Kibwana aliyepata kura 8 Sawa na asilimia 7.4 na Janken Kasambala mwenye kura 38 sawa na aslimia 35.5.

Baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya NRA, Mahona alimchagua  Khamis All Hassan kutokea Zanzibar kuwa mgombea mwenza

Katika Mkutano huo, NRA wamempitisha pia Khamis F Mgau kuwa mgombea wa Urais Zanzibar akipata kura 75 sawa na asilimia 68.8  ya kura zote.

Fakhi amewapiku wapinzani wake  Marshed Humud akipata kura 23 sawa na asilimia 21.1 na Amina Rashid akipata kura 4 sawa na aslimia 6.4 huku kura 4 zikiharibika.

Mkutano huo Mkuu ulihudhuriwa na Msajili wa Vyama vya Siasa   Sixty Nyahoza  na viongozi mbalimbali kutoka vyama vya siasa nchini.

Nyahoza amewapongeza NRA kwa kufanya uchaguzi uliokuwa wa haki na demokrasia kwa wajumbe kumchagua mgombea wao wa Urais kwa mwaka wa Uchaguzi 2020.

Aidha, amewapongeza wagombea wote wanaowania nafasi ya Urais kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NRA wamefanya mkutano mkuu wa kuwapitisha wagombea wa nafasi ya Urais pamoja na kuwataka wagombea nafasi ya Ubunge na Udiwani wa maeneo mbalimbali majina yao yapitishwe na Kamati za chama za Kata ili kupelekwa tume ya Uchaguzi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2