CRDB YAZINDUA MFUMO WA UTOAJI MAONI KIDIGITALI | Tarimo Blog


Charles James, Michuzi TV

TAASISI za Fedha nchini zimetakiwa kuboresha huduma zake kwa kwenda na mabadiliko ya kisayansi ikiwa ni pamoja na kuhama kufanya kazi kwa mfumo wa analojia na kwenda kidigitali.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM), Prof Faustine Bee wakati akizindua mfumo wa kielektroniki wa utoaji maoni kwa wateja wa Benki ya CRDB.

Prof Bee ameipongeza benki hiyo kwa kufanya mabadiliko hayo ambayo anaamini yatawawezesha wateja wao kutoa maoni yao bila kumuogopa mtu na kwa uwazi zaidi.

Kifaa hicho kilichozinduliwa kimepewa jina la 'feedback' na kitakua kikitumika kutolea maoni ambapo Meneja wa CRDB Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro anaamini kitawapa Uhuru zaidi wateja kutoa maoni bila kumuonea aibu mtu.

" Niwapongeze sana ndugu zetu wa CRDB kwa kubuni mfumo huu ambao unaonesha jinsi gani benki hiyo inazidi kukua na kujitofautisha na taasisi zingine, niwasihi mzidi kujipanua kiteknolojia na kwenda mbali zaidi.

Kama kawaida yenu mmekua wabunifu katika mambo mengi, mlikuja na mfumo wa kuwakopesha wanafunzi ambao hawana fedha jambo ambalo limewasaidia watoto wengi wa kimaskini na pindi pesa zao zikiingia wanakatwa kidogo kidogo, nitoe rai kwa mabenki mengine kuja na mfumo kama huu," Amesema Prof Bee.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro amesema benki hiyo itaendelea kuwahudumia watanzania kwa spidi na kwa kasi kama ambavyo Rais Magufuli amekua akisisitiza.

" Tutaendelea kutoa huduma zetu kwa kasi hii hii tuliyonayo, ubunifu kwetu ndio mahala pake, tutazidi kuwafikia wateja wetu kwa namna ya pekee hasa kwa mfumo wa digitali ambapo dunia ndio ilipofikia," Amesema Chabu.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu Dodoma (UDOM), Prof Faustine Bee akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya CRDB tawi la Udom.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM, Prof Faustine Bee akiwa na Meneja wa CRDB kanda ya kati wakiwa wameshika vifaa maalum vya kielektroniki vya wateja kutolea maoni.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha UDOM, Prof Faustine Bee (katikati) akikata utepe kuashiria kuzindua mashine maalum za utoaji maoni kwa njia ya kielektoniki iliyozinduliwa na Benki ya CRDB.
 Meneja wa CRDB Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kifaa maalum cha utoaji maoni kwa wateja wa Benki hiyo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2