Na Amiri Kilagalila,Njombe
Madereva wa bodaboda mjini Njombe wametakiwa kuacha tabia ya kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi Pamoja kuifanya kazi hiyo kuwa rasmi kwa kupata elimu katika vyuo vinavyotambulika na serikali ili kuepusha ajali zisizo za lazima.
Wito huo umetolewa na COPLO Marwa Kisyeri pamoja na DTO Godlisen Ndosa kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Njombe kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Njombe wakati wa kuhitinisha kampeni ya kukomesha ajali barabarani kata ya Mjimwema iliyoratibiwa kwa ushirikiano na chuo cha ufundi cha Tagaste kilichopo mjini hapa na kumbatana na zoezi la gawaji zawaji kwa dereva bora wa piki piki aliyepatikana kupitia zoezi hilo.
“Tumeona wapate elimu ili tuone je zile ajali zinazopatikana kila siku zinapungua au la,na hatutaki kusikia ajali kwasababu zinarudisha nyuma maendeleo yetu”alisema Ndosa
Katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja,mkuu wa chuo cha udereza na ufundi TAGASTE kilichopo mji mwema halmashauri ya mji wa Njombe ELENEUS MGIMBA.Amewakumbusha madereva bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani Pamoja na kuhamasishwa kupata elimu ya udereva
“Tukianza na hili kundi la bodaboda tumeona ajali nyingi zinaonekana zinasababishwa na hawa boda boda,kwa hiyo sasa tunajitahidi kutengeneza mazingira ya kuwafikia kwasababu kundi kubwa wanakuwa hawajapita kwnye vyuo na kupata misingi ya udereva wao”alisema Eleneus Mgimba
Serikali ya mtaa wa Mjimwema kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa LEONARD ETEN MKUPI inasema mtaa huo baadhi ya Watoto wamepoteza Maisha na wengine kupata ulemavu kutokana na ajali na kuwa elimu ndio njia pekee itakayokomesha ajali.
“Naamini kwa mafunzo haya ajali zitapungua kwa kiasi kikubwa sana,tumepoteza watoto wawili pale mji mwema shule ya msingi mmoja amepata ulemavu lakini mwingine tumeshampoteza kwasababu ya kuendesha vyombo hivi bila utaratibu,lakini kwa mafunzo haya naamini vijana watakuwa wamepata mafunzo na kuepusha ajali”alisema Leonard Mkupi
Kwa niaba ya madereva wa Boda boda,mwenyekiti wa usafirishaji kupitia vyombo hivyo Bwana Fredy Ndelwa amesema wapo tayari kuendelea kutii kila wanachoelekezwa kwa kuwa usafiri huo ndio unaotumika kwa kiasi kikubwa.
“Tunatabia ya kusikiliza nini tunambiwa na tupo tayari kutii kwasababu usafiri wa boda boda unakubalika na unaingia mahali popote pale kwa hiyo sisi tunapenda sana elimu”alisema Fredy Ndelwa
Washindi watatu katika zoezi la kumpata dereva bora wa usafiri huo wa boda boda kata ya mji mwema wamekabidhiwa zawadi mbali mbali ikiwemo kofia ngumu za kujikinga na majeraha kichwani inapotokea ajali.

Godlisen ndosa kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilaya ya njombe kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa njombe,akizungumza na kutoa zawadi ikiwemo kofia ngumu kwa madereva bor wa boda boda mjini njombe walipotikana katika mchakato ulioendeshwa na chuo cha ufundi tagaste.
Baadhi ya madereva wa piki piki waliofika katika hafla fupi ya kumkabidhi zawadi mshindi na dereva bora wa boda boda.
E:Mkuu wa chuo cha udereva na ufundi magari ndugu ELENEUS MGIMBA akizungumza na vyombo vya habari sababu ya kuanzisha mchakato huo ikiwemo kuendelea kutoa elimu ya usalama kwa madereva wa boda boda kuepusha ajali.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment