KINONDONI YAKABIDHI VYOMBO VYA USAFIRI WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 91 KWA VIKUNDI VYA VIJANA | Tarimo Blog








Bodaboda zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa vikundi vya vijana kutokana na fedha za mkopo wa asilimia 10 kwa makundi ya vijana, Wanawake na watu wenyeulemavu.



Bajaji zilizitolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa vikundi vya vijana kutokana na fedha za mkopo wa asilimia 10 kwa makundi ya vijana, Wanawake na watu wenyeulemavu.



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na vikundi vya vijana wakati alipokuwa akiwakabidhi bodaboda na bajaji vilivyotokana na mikopo ya asilimia 10 katika makundi hayo.



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo wa kwanza kushoto, Kaimu Mkurugenzi Kiduma Mageni pamoja na Mratibu wa Mikopo Bi. Leah Momba akifuatilia taarifa ya utoaji wa mikopo hiyo iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Bi. Halima Kahema.



Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Kiduma Mageni akizungumza na vijana walionufaika na mikopo ya asilimia 10 inayolewa na Halmashauri hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Daniel Chongolo na kulia ni Mratibu wa Mikopo Bi. Leah Momba.



Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Bi. Halima Kahema akizungumza na viajana walionufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri hiyo wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo.



…………………………………………………………………………

Manispaa ya Kinondoni leo imekabidhi vyombo vya moto vya usafiri Bodaboda na Bajaji vyenye thamani ya shilingi milioni 91 kwa vikundi 21 vya vijana kwa lengo la kuwawezesha katika kujikwamua kiuchumi.

Akikabidhi vyombo hivyo ambavyo ni bodaboda 20 na bajaji sita, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa uwezeshwaji huo unatokana na fedha za makusanyo ya ndani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli la kutenga asilimia 10 ya bajeti ya Halmashauri kila mwaka kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

“Rais wetu Dk. Magufuli alielekeza fedha hizi ambazo wanapewa makundi haya, zitolewe bila riba ili kila mmoja awe mnufaika, nitumie fursa hii kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kusimamia maelekezo haya vizuri na leo hii tunaona vijana wetu wakinufaika na mpango huu” amesema Mhe. Chongolo.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu. Kiduma Mageni amesema kuwa Kinondoni ni Halmashauri inayotekeleza kwa vitendo na kwamba inazingatia uwezeshwaji wa vijana katika sekta zote za Uchumi na za kijamii na kufafanua kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2019/ 2020 kiasi cha shilingi Bilioni 3.3 kilitengwa kwa vikundi vikundi 722.

Ameongeza kuwa katika fedha hizo, vikundi 510 tayari vimeshanufaika na mkopo, wakati vingine 212 vikiwa kwenye mchakato wa mwisho wa kupatiwa fedha hizo na kwamba inaendelea kuhamasisha jamii juu ya uwepo wa asilimia 10 kwa ajili ya kuwezesha na kuinua Wananchi kiuchumi kwa akuzingatia ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2