Shirika la LifeWater International limetoa msaada wa ndoo 150 na stendi zake kwa ajili ya kunawia mikono ili kuendeleza mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona na kuimarisha usafi wa mwili na mazingira katika shule 12 za msingi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi ndoo hizo leo Alhamis Julai 24,2020 katika kata ya Mwalukwa, Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga ndugu Benety Malima amesema, licha ya maambukizi ya COVID – 19 kupungua lakini bado upo umuhimu wa kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
“Shirika letu la LifeWater International linajihusisha na masuala ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Afya na Usafi wa Mazingira. Tumetoa ndoo hizi zenye ujazo wa lita 60 kila moja zikiwa na stendi zake ili wanafunzi waendelee kuishi katika hali ya usafi wa wa mwili na mazingira na kuepuka magonjwa mbali mbali”,alieleza Malima.
Alisema kupitia mradi wao wa Maji Safi na Salama pamoja na Usafi wa Mazingira, wameamua kugawa ndoo za kunawia mikono ambapo kwa awamu ya kwanza watagawa ndoo na stendi 150 kwenye shule za msingi ili kuwezesha wanafunzi kuchukua tahadhari dhidi ya COVID – 19 na kuwaepusha wanafunzi kupata magonjwa mengine ikiwemo homa za matumbo, minyoo na kuhara.
Alisema ndoo hizo zitagawiwa katika shule za msingi 12 zilizopo kwenye kata za Mwalukwa, Mwamala na Mwantini ambazo ni Bulambila,Ng’hama,Ng’walukwa A,Ng’walukwa B,Bushoma, Hinduki, Jimondoli,Kilimawe,Bugogo, Bunonga,Igegu na Ibanza.
Aidha alifafanua kuwa shule hizo zipo kwenye mpango wa shirika la LifeWater International wa ujenzi wa miundo mbinu ya vyoo vya kisasa kulingana na mwongozo wa serikali pamoja na kupeleka miundo mbinu ya maji katika shule na kuendelea kutoa elimu kuhusu maji safi na salama na usafi wa mazingira.
Kwa upande wake, Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bashiri Salum alilishukuru shirika la LifeWater International kwa kutoa msaada wa vifaa hivyo vya kunawia mikono ambapo na kutumika kuchukua tadhari dhidi ya COVID – 19 vitasaidia kuimarisha hali ya usafi wa mwili na mazingira shuleni.Aidha aliwataka walimu na wanafunzi kutunza vifaa hivyo vya kunawia mikono huku akiwahamasisha kufanya usafi mara kwa mara kwenye vyoo, ofisi na madarasa yao.
Wakipokea vifaa hivyo,vilivyogawiwa leo katika kata ya Mwalukwa, walimu wakuu katika shule za msingi Bulambila,Ng’walukwa A, Ng’walukwa B na Ng’hama waliahidi kutunza vifaa hivyo na kuendelea kuwahamasisha wanafunzi wao kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akikagua ndoo 150 zenye ujazo wa lita 60 kabla ya kuanza zoezi la kuzigawa leo Alhamis Julai 24,2020 katika shule za msingi 12 zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ajili ya kunawia mikono ili kuendeleza mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona na kuimarisha usafi wa mwili na mazingira. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa sehemu ya ndoo na stendi za kunawia mikono zilizotolewa na Shirika la LifeWater International.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akinawa mikono kwa kutumia ndoo na stendi katika shule ya Msingi Ng'hama iliyopo katika kata ya Mwalukwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Shule hiyo hiyo imepatiwa ndoo na stendi 11.
Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bashiri Salum (kushoto) akiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi Ng'hama namna ya kunawa kwa usahihi ukitumia maji tiririka na sabuni.
Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bashiri Salum (katikati) akiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi Ng'hama namna ya kunawa kwa usahihi ukitumia maji tiririka na sabuni.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Mwalimu Mkuu Msaidizi shule ya Msingi Ng'hama, Erasto Langston Mbalawata (kushoto). Shule hiyo imepewa ndoo na stendi 11 za kunawia mikono.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Mwalimu Mkuu Msaidizi shule ya Msingi Ng'hama, Erasto Langston Mbalawata (wa pili kushoto). Wa kwanza kushoto ni Mwalimu wa usafi shule ya msingi Ng'hama Sophia Mathew. Wa kwanza kulia ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Wilson Mwita akifuatiwa na Afisa Mtendaji Kata ya Mwalukwa, Monica Mussa.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Dada Mkuu wa shule ya Msingi Ng'hama.
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Ng'hama akionesha wanafunzi wenzake namna ya kunawa mikono kwa usahihi.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Bulambila iliyopo katika kata ya Mwalukwa , John Wales (kushoto). Shule hiyo imepewa ndoo na stendi 9 za kunawia mikono.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Mwalimu Mkuu Msaidizi shule ya Msingi Ng'walukwa A iliyopo katika kata ya Mwalukwa , Zainu Hamoud (kulia). Shule hiyo imepewa ndoo na stendi 7 za kunawia mikono.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Ng'walukwa B iliyopo katika kata ya Mwalukwa B , Nagomelwa Edson (kushoto). Shule hiyo imepewa ndoo na stendi 6 za kunawia mikono.
Meneja wa Shirika la LifeWater International Mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akimkabidhi ndoo na stendi ya kunawia mikono Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Ng'walukwa B iliyopo katika kata ya Mwalukwa B , Nagomelwa Edson (kushoto). Wengine ni walimu wa shule hiyo ambayo imepewa ndoo na stendi 6 za kunawia mikono. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment