TASAC kuendelea na mapambano ya uchafuzi katika bahari na maziwa | Tarimo Blog


 Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Emmanuel Ndomba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana  na  maadhimisho ya siku ya Bahari Afrika ambayo huadhimishwa Julai 25
 Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dk. Erick Masami akizungumza kuhusiana na uandaji wa mabaharia katika chuo hicho katika kuweza kufkia malengo ya utojaji wa huduma katika shughuli za bahari.
Katibu wa  Chama cha Wanawake Mabaharia  (Womesa) Dkt.Devotha Mandanda akizungumza umuhimu wanawake kupenda kusoma ubaharia.

 
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema litaendelea kupambana na uvuvi haramu unaotumia baruti na sumu baharini, utupaji wa taka za plastiki, biashara ya mafuta ya magendo inayofanyika majini, uharamia pamoja na ujambazi wa silaha dhidi ya meli.

Katika mapambano hayo ni pamoja kupambana na umwagaji wa mafuta baharini, biashara ya silaha, dawa za kulevya, magendo na kuongeza kuwa watazingatia malengo hayo kama yalivyoainishwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika (CAU) kwenye maeneo ya bahari na maziwa.

Hayo yote yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Emmanuel Ndomba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Bahari Afrika ambapyo huadhimishwa Julai 25 ya kila mwaka .

Katika maadhimisho hayo wafanyakazi wa Shirika hilo kwa kushirikiana na wadau wengine watafanya shughuli mbalimbali za kijamii zisizokuwa na mikusanyiko kwa lengo la kuchukua tahadhari ya virusi vya Corona.

Ndomba amesema Serikali itazingatia pia katika ufanyaji wa utafiti, ubunifu, uendelezaji wa uchumi endelevu wa bahari, utafutaji wa mafuta na gesi baharini, tabia nchi, ulinzi wa mazingira, uhifadhi pamoja na uchukuzi salama baharini.

"Malengo ya maadhimisho ni muhimu kwa taifa katika kuongeza uwezo na ufanisi wa kutumia rasilimali zinazopatikana kwenye bahari, maziwa na mito ili kukuza uchumi wa nchi huku tukiendelea kushirikiana kikamlifu kwa kutekeleza maazimio haya, mikataba ya kimataifa itakayorodhiwa na Serikali yetu ya Tanzania, " amesema Ndomba.

Amesema Tanzania ni nchi yenye ukanda mkubwa bahari ya Hindi wenye urefu wa Kilomita 1426 kutoka mkoa wa Tanga mpaka mkoani Mtwara, pia inazungukwa na maziwa makubwa kama ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa.

"Mazingira haya yanavutia kuyatumia vema kwa kuwa na sera, sheria na utekelezaji mzuri ambao utapelekea kuwa nchi yenye ulinzi, usalama na uchumi wa bahari ili kuendelea kuvutia na kuinua biashara ya meli ambayo ni endelevu na kkuwa chachu ya kuibua fursa kwa wadau, wananchi na wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi kwenye sekta ya bahari”.

"Matokeo chanya tuliyoyapata ni baada ya Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar kuendelea kuwekeza katika miradi mikubwa nchini ikiwemo miradi inayoendelea kutekekezwa ambayo ni upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, ghati ya Kabwe na Kasanga katika ziwa Tanganyika na ujenzi wa Chelezo ya Meli Mwanza South, ziwa Victoria, ujenzi wa meli kubwabya abiria na mizigo na ukarabati mkubwa wa Meli ya MV. Victoria na Mv. Butiama, ununuaji wa meli ya mizigo na abiria MV. Mapinduzi II na MT. Mkombozi II ambayo ni ya kubebea mafuta na gesi, hivyo kuna fursa nyingi za kiuchumi zimeletwa na miradi hii iliyopo na ijayo," amesema Ndomba.

Amesema maadhimisho ya mwaka huu yataadhimishwa kwa kauli.mbiu inayosema 'ubunifu katika matumizi endelevu ya bahari'.

"TASAC, Mamalaka ya Bahari Zanzibar na wadau wote tunaadhimisha siku hii kwa kutumia njia ya Tehama na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zisizokuwa na mikusanyiko ya watu wengi kwa lengo la kuchukuwa tahadhari ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19)," amesema

Naye Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dk. Erick Masami amesema anatoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri majini kujitokeza kwa wingi kusoma katika chuo hicho ilikupata ujuzi wa kutosha wa namna ya kukutumia vyombo hivyo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2