MAAFISA WAANDIKISHAJI WA TASAF WATAKIWA KUWA WAADILIFU KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI KAYA ZAWANUFAIKA | Tarimo Blog

Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani TASAF Makao Makuu, CPA-Christopher Sanga,akikagua zoezi la uhakiki wa Wanufaika wa Mpango wa  TASAF Kipindi cha pili Awamu ya Tatu kwenye Kata ya Chamwino.

MAAFISA  wawezeshaji wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, wametakiwa  kuwa waadilifu wakati wa  zoezi la uhakiki wa Kaya za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  (TASAF) katika utekelezaji  wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.

Hayo yameelezwa leo Julai 22,2020  na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani TASAF Makao Makuu, CPA-Christopher Sanga, wakati wa ufunguzi wa zoezi hilo la Uhakiki lililoanza leo kwenye Kata 6 Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Sanga, amewataka wawezeshaji hao kuwa makini wakati wa kuhakiki taarifa za Walengwa ili  kufanikisha zoezi la uhakiki wa kaya za walengwa wa TASAF   na kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii ya kuwepo Walengwa hewa.

Aidha, CPA Sanga, amewataka wawezeshaji hao ambao ni watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuwa waaminifu na waadilifu wakati wa zoezi hilo.

“Hatua hii ni muhimu sana kwetu . tunawaomba Maafisa wetu mmepewa kazi hii kwa uaminifu tukiamini kwamba mtaitendea haki ili kuwapata walengwa halisi na kuondoa dhana ya walengwa hewa, mfuate miongozo ,kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali ili kufanikisha zoezi hili limalizike kwa ufanisi wa hali ya juu sana, mmeshapata mafunzo hatutegemei kwamba mtatuangusha fanyeni kazi shirikianeni vyema na Wenyeviti wa Mitaa ambao wao ndio wenye wananchi hao mitaani ili zoezi letu lifanikiwe “Amesema Sanga.

Sanga ameeleza kuwa Serikali iliamua kuendelea na kipindi cha pili katika awamu ya tatu ya TASAF ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi kwani katika kipindi cha kwanza cha TASAF awamu ya tatu,  idadi ya kaya zilizofikiwa ni sawa na 70 % ya Kaya zenye mazingira duni nchini, hivyo  kipindi cha pili cha TASAF awamu ya tatu kitatekelezwa katika Halmashauri zote 185 Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar ambapo jumla ya  kaya milioni moja laki nne na nusu zenye jumla ya watu zaidi ya milioni 7 kote Nchini zitafikiwa ikiwa ni ongezeko la kaya laki tatu na nusu.

Amewatahadharisha  wawezeshaji hao kufanya  kazi kwa  waadilifu kwani wakienda kinyume   kwani watawajibishwa endapo itabainika uwepo wa Kaya zisizo na sifa katika eneo walilofanya kazi .

Ikumbukwe kwamba zoezi hilo  la kuhakiki Kaya za wanufaika wa TASAF limeanza leo Julai 22, 2020 katika Kata 6 za awali za Manispaa ya Morogoro zikiwemo Kata ya Kihonda Maghorofani, Bigwa, Boma, Chamwino, Kiwanja Cha Ndege pamoja na Kauzeni ambapo zoezi hilo litaendelea tena hadi kuzifikia Kata zote 29 za Manispaa ya Morogoro.

Kabla ya zoezi hili la Uhakiki wa Kaya za Wanufaika wa TASAF , kulikuwepo na Semina ya Wawezeshaji ya kuwajengea Uwezo iliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Julai 20-21, 2020 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.

Naye Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Feliciana Katemana,amesema zoezi hilo limeanza kwa matumaini kwani hata idadi ya walengwa waliojitokeza imekuwa na uwiano mzuri.

“”Zoezi limeonyesha matumaini makubwa, hapa Kata ya Kihonda Maghorofani kuna jumla ya Walengwa 61 lakini kwa idadi tunayoiona imeonesha kwamba mwitiko umekuwa mkubwa sana , hata Kata ya Chamwino watu wameitika sana kikubwa niwaombe Wataalamu wangu waendeshe zoezi hili kwa umakini sana hata kama kuna dosari zitajitokeza zitakuwa ndogo ndogo ambazo naamini wakishrikiana vyema na Wenyeviti wa Mitaa watazitatua bila wasiwasi” Amesema Katemana.

Katemana amesema mpango wa  kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF Manispaa Morogoro utalenga jumla ya Walengwa 2793 katika Kata 29 ikiwamo Mitaa 164. Ratiba ya Zoezi la Uhakiki ni kama ifuatavyo;
Na
KATA
TAREHE

1. KICHANGANI
23/07/2020

2. KILAKALA
23/07/2020

3. KINGOLWIRA
23/07/2020

4. LUHUNGO
23/07/2020

5. LUKOBE
23/07/2020

6. MAFIGA
23/07/2020

7.MAGADU
23/07/2020

8. MAZIMBU
23/07/2020

9. MBUYUNI
23/07/2020

10. MINDU
24/07/2020
11. MJI MKUU
24/07/2020

12. MJI MPYA
24/07/2020

13.MKUNDI
24/07/2020

14. MLIMANI
24/07/2020

15. MWEMBESONGO
24/07/2020 

16. MZINGA
24/07/2020

17. SABASABA
24/07/2020

18. SULTAN AREA
24/07/2020

19.TUNGI
24/07/2020

20. UWANJA WA TAIFA
24/07/2020

21. MAFISA
24/07/2020

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2