MABALOZI ‘WAMLILIA’ RAIS MSTAAFU MZEE MKAPA | Tarimo Blog



Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa aliyeaga dunia Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam. Mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyomfahamu Rais Mstaafu Mzee Mkapa wakati alipokuwa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam Balozi wa Finland chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin MkapaBalozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa Marehemu jijini Dar es Salaam.

************************************

Baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wamejitokeza kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliyeaga dunia Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam ‘wakimlila’ na kumuelezea kwa mema mengi aliyoyafanya wakati wa uhai wake.

Mabalozi hao walianza kuwasili nyumbani kwa Mzee Mkapa kwa nyakati tofauti ambapo mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo baadhi yao wakaelezea walivyoguswa na msiba.

Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa amemuelezea Mzee Mkapa kuwa alikuwa mtu makini na aliyependa masuala ya kidiplomasia.

“Nimekuja hapa kwa niaba ya Serikali ya Misri kuja kutoa pole kwa kuondokewa na Mzee Mkapa kiongozi mchapakazi kwa taifa la Tanzania na alikuwa kiongozi aliyeinua uchumi wa taifa ambapo chini ya uongozi wake Tanzania iliingia katika ubinafsishaji na utandawazi”, Amesema Balozi Abulwafa.

Ameoneza kuwa Mzee Mkapa atakumbukwa na wanadiplomasia wengi duniani kwani alikuwa kiongozi aliyependa amani ambapo enzi za uhai wake alisuluhisha mauaji ya kimbari katika nchi za Rwanda na Burundi pamoja na kurejesa amani katika nci za Sudan, Kongo DRC, Zimbabwe na Kenya.

“Tutamkumbuka kwa upendo na uchapakazi wake uliokuwa umetukuka na kuonesha matunda ya amani na mandeleo kwa Tanzania na Afrika Mashariki”, Amesema Balozi Abulwafa.

Kwa upande wake mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald amemuelezea Rais Mstaafu Mzee Mkapa kuwa alikuwa rafiki mkubwa wa Ireland, na ambaye aliyeendeleza na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ireland ambao hadi sasa upo imara.

“Kwetu sisi kama Serikali ya Ireland tumeguswa sana na msiba huu, kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi na mpenda amani….daima tutamkumbuka kwa mema yaka na uchapaji kazi wake ulioiletea Tanzania maendeleo. Tulimfaamu vizuri alikuwa kionozi mpenda maendeleo na amani……kwetu sisi ni pigo kubwa sana kwa kifo chake.

Baadhi ya mabalozi waliofika na kusaini kitabu cha maombolezo ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi, Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa, Balozi wa Finland chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan, Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi pamoja na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Ahamada Elbadaour Mohamed

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2