MEMBE RASMI KUWANIA URAIS WA TANZANIA KUPITIA ACT WAZALENDO | Tarimo Blog


Na Bakari Madjeshi,  Michuzi TV

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Bernard Membe rasmi amechukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Membe amechukua Fomu hiyo ya kuwania Urais katika Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam kufuatia ombi la Wanachama na Mwenyekiti,  Maalim Seif Sharif Hamad kumuomba kuwania Urais.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Fomu na Katibu Mkuu wa Chama,  Ado Shaibu,  Membe amesema uchukuaji wa Fomu hiyo ni mwanzo wa harakati za kuwania urais nchini,  amesema  atazungumza kwa kirefu zaidi siku ambayo atarudisha Fomu hiyo.

"ACT Wazalendo inakwenda chap chap chap! hatuwezi kuchelewa, nitatekeleza miongozo ya Fomu hii, na nitaijaza fomu hii vizuri sana kwwnye Nukta nitaweka kubwa,  herufi ndogo nitaweka ndogo ili asipite mtu akisema sikujaza vizuri fomu hii.

nitatema cheche siku ambayo nitarudisha fomu hii,  hapa nina mzigo kweli kweli",  amesema Membe.

Membe amesema ameona jina lake la kwanza katika orodha ya wanaowania urais kupitia Chama hicho, amesema anashukuru kuwaanza yeye kuchukua Fomu hiyo hata hivyo wengine wanaruhusiwa kutokana na Demokrasia.

"Nitaheshimu kila mnalolitaka na ndio maana sikutaka kabisa kuchelewesha kutoa majibu,  Wakubwa wako wanavyokwambia na kukuliza swali! Swali limeulizwa leo limejibiwa",  amesema Membe.

Amesema anashukuru sana kwa kitendo cha Uongozi wa Chama, Wanachama wote kwa kumuunga mkono sambamba na Kiongozi wa Chama,  Zitto Kabwe na Mwenyekiti, Maalim Seif Sharif Hamad.
  Katibu mkuu ACT Wazalendo Ado Shaibu akimkabidhi Mhe Bernard Membe begi lenye fomu za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho
 Mhe.Membe akiwaonesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani),akiwaonesha begi lenye fomu za kuwania Urais mara baada ya kukabidhiwa.Picha na Michuzi JR -MICHUZI MEDIA.
 Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne,Mhe  Bernard Membe akizungumza na Waandishi wa Habari leo mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo. Membe amechukua Fomu hiyo ya kuwania Urais katika Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam kufuatia ombi la Wanachama na Mwenyekiti,  Maalim Seif Sharif Hamad kumuomba kuwania Urais.

Mhe. Membe alipokuwa akiwasili kwenye  ofisi za Makoa Makuu ya chama cha ACT Wazalendo zilizopo Magomeni,Kinondoni jijini Dar kuchukua Fomu  ya kuwania Urais  kufuatia ombi la Wanachama na Mwenyekiti,  Maalim Seif Sharif Hamad kumuomba kuwania Urais
  Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne,Mhe  Bernard Membe akisaini fomu ya kugombea Urais ndani ya chama hicho,kulia ni Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2