OFISA WA BENKI KIZIMBANI KWA UTAKATISHAJI | Tarimo Blog

 Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

OFISA Wa Benki ya Baclacys, Gabriel Tesha (35) mkazi wa Tabata Kinyerezi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya wizi na utakatishaji wa fedha kiasi cha sh. milioni 64.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa  na wakili wa serikali  Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga imedai Oktoba Mosi 2017 na Mei 31,2018 huko katika maeneo ya Benki ya Baclacys jijini Dar wa Salaam Tesha akiwa kama ofisa wa ukadiriaji fedha, wa benki hiyo aliiba Sh milioni 64.

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa Oktoba Mosi 2017 na Mei 31,2018 maeneo ya Benki ya Baclacys jijini Dar wa Salaam mshtakiwa Tesha akiwa kama ofisa wa ukadiriaji fedha mshitakiwa huyo alijihusisha na miamala ya Sh milioni 64 alizoingiza na kutoa fedha katika akaunti ya Shilingi na USD anazomiliki  huku akijua kuwa fedha hizo ni zaonla kosa la wizi.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kuwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 29, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa, mshtakiwa amerudishwa rumande kwa sababu mashtaka hayo hayana dhamana kisheria.

Mwisho

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2