RAIS Dk.John Magufuli amesema waliochukua fomu za kuwania ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wapo 10,367 na kati ya hao waliokamilisha taratibu zote zinazotakiwa ni 10,321 huku akitumia nafasi hiyo kuomba mchakato wa kuhesabu kura za maoni uwe wa wazi.
Akizungumza leo Julai 20,2020 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa kuwaapisha viongozi wateule ambao wanajaza nafasi za viongozi ambao wameomba ruhusa kwa ajili ya kwenda kuomba ridhaa ya kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
"Nawapongeza wateule wote ambao wamepata nafasi hizi, ni matumaini yangu mtakwenda kutekeleza majukumu yenu vema, ni kweli kwamba mmepata nafasi hizi kwasababu ya fursa ambazo zimepatikana, na ninaimani kubwa na niny.
"Waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali kwa taarifa ambazo nimepewa leo hii ni 10,367.Katika hao waliokamilisha taratibu zote ni 10,321 kwa hiyo wale ambao hawakurudisha ni 46 katika nchi nzima, kwa hiyo unaweza kuona ni watu wengi sana wamejitokeza, haijawahi kutokea.
"Kwa mfano kwenye ubunge tu wamejitokeza hao 10,367, nawapongeza wote ambao wamejitokeza kwenda kuomba nafasi mbalimbali. Kura za maoni zitaanza leo na kesho na matumaini yangu kura hizo zitasimamiwa kwa uwazi, bila mizengwe yoyote,"amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa ni matumaini yake viongozi wa Chama chake cha CCM ambao wasimamia mchakato huo wa kura za maoni basi watazihesabu hadharani kwani uwazi utasadia kuendelea kujenga uwazi. Kura hizo zihasabiwe hadhari mbele ya wajumbe, kila mmoja aweze kuona.
Hata hivyo amesema kuwa kwa siku za karibuni wamekuwa wakikutana kwa ajili ya kuapisha viongozi mbalimbali, lakini anaamini sasa hiyo haitakuwepo tena baada ya uapisho ambao umefanyika leo.
"Najua hii huenda ikatokea huko mbele ya safari lakini ni ninyi ambao umepata nafasi hizi ndio mmeshazijaza tayari labda kama kuna mwingine atakwenda kutangaza nia kwingine."
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment