Na Mwandishi Wetu, TV
SIMBA raha sana!Ndivyo unavyoweza kuzungumzia ushindi wa mabao 5-1 walioupata timu ya Simba dhidi ya timu ya Alliance ikiwa ni mechi yao ya mwisho kwa msimu huu kucheza jijini Dar es Salaam.
Ufundi mwingi,umahiri,uwezo wa kumiliki mpira na kila aina ya udambwi dambwi katika soka umeifanya Simba kuibuka na ushindi huo mnono.Pamoja na umakini wa wachezaji wa Alliance bado haikuwa njia ya kujinasua na kipigo hicho.
Mchezo huo ambao umechezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku kombe likiwa uwanjani ambacho Simba wameamua kwenda Uwanjani kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki wao, ulikuwa wa vuta ni kuvute lakini ukionesha uwezo mkubwa wa wachezaji wa Simba.
Iko hivi, Simba walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambualiaji wake machachari Medi Kagere ambaye alifunga kwa mkwaji wa penalt uliomshinda mlinda mlango wa timu ua Aliiance .Hata hivyo Alliance walifanikiwa kupata bao la kusawazisha na hivyo dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko kwa kumtoa Jonas Mkude na kisha kumuingiza Mzamiru Yasin.Pia alitoka Francis Kahata ambaye kwenye mchezo wa leo ameonesha ufundi mwingi alionao wa kusakata kabumbu kwenye ardhi ya Tanzania.
Uwezo wa Simba katika mchezo huo uliifanya Simba kupata bao la pili lililofungwa na Medie Kagere.Kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo kasi ya wachezaji wa Simba ilivyokolea na hivyo Luis Miquissone aliipachikia timu yake bao la tatu.Hata hivyo Mickson alitoka na kuingia Hassan Dilunga.
Wakati mchezo huo ukiendelea wapo baadhi ya mashabiki wa soka waliokuwa wakitamani mpira uendelee kutokana na burudani iliyokuwa ilitolewa uwanjani hapo kutoka kwa wachezaji wa timu zote mbili.
Hata hivyo kipigo kwa Alliance kiliendelea na hivyo kuiwezesha Simba kupata bao la nne kupitia kwa mchezaji wake Deo Kanda ambaye aliingia kipindi cha pili cha mchezo.Alifunga bao hilo baada ya kupokea mpira uliopigwa na Kagere.
Simba hawakuishia hapo kwani waliendelea na mashambulizi ya kasi dhidi ya wapinzani wao na hatimaye kupata bao la tano kupitia mshambuliaji wake Hamis Ndemla.Hivyo hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Simba wameibuka na ushindi huo Kombe lao likiwa uwanjani.
Kwa kukumbusha tu Simba leo ndio mechi yake ya mwisho kuchezwa katika viwanja vya Dar es Salaam kwani sasa inaelekea mkoani Tanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Coasal Union ya jijini humo.
Haha Hi yo Simba baada ya kumalika kwa mchezo wake dhidi ya Alliance wachezaji walikwenda kwa mashabiki kama ishara ya kushangilia nao pamoja ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara ukiwa ni ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment