Stamico yasaini mkataba wa ukandarasi wa uchorongaji miamba na Kampuni ya Madini ya GGM | Tarimo Blog

Waziri wa Madini Dotto Biteko wakati akiongea kwenye tukio hili la utiaji sahihi kati ya STAMICO na GGM.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico, Meja Generali mst M.J Isamuhyo akizungumza wakati wa tukio hili.
 Mkurugezi wa GGM Bwana Richard Jordison naye akiweka sahihi kwenye mkataba wa Kandarasi ya uchorogaji miamba na STAMICO.
Wakuu wa mashirika haya mawili wakionesha mikataba baina yao baada ya kusainiwa.
Viongozi Wakuu wa STAMICO na GGM wakibadilishana mkataba mbele ya wanasheri wao na Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO. Mej Generali mst M. J Isamuhyo

 STAMICO  imesaini mkataba wa kandarasi ya uchorogaji miamba na kampuni ya Madini ya GGM. Makubaliano hayo yamefanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Geita na kuhudhuria na viongozi mbali mbali wa Serikali na GGM. Mgeni Rasmi kwenye tukio hili alikuwa, Waziri wa Madini,  Doto Mashaka Biteko. 

Tukio hiko lilihudhuriwa  na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Eng Robert Gabriel, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof Simon Msanjili, RAS, Mkuu wa Wilaya  na Viongozi na wafanyakazi kutoka STAMICO na GGM. Katika hotuba yake Mheshimiwa Waziri amelipongeza sana STAMICO kwa kazi nzuri wanayofanya kwa hasa katika kuchangia pato la Taifa na Kuhusu mkataba na GGM aliwaelekeza STAMICO kufanya  kazi kwa bidii na kwa uaminifu na kwa kiwango Cha juu ili  kujenga jina la STAMICO. 

“Kandarasi Hii ni ya kwanza kwa hivyo  tufanye kazi hii kwa viwango vya Juu kwa  kutumia ujuzi  wetu wote. Kandarasi Hii ni Karata na tuicheze vizuri najuwa tutashida kwani STAMICO ina uongozi Bora na wafanyakazi waliosoma na wanaojuwa kufanya kazi hii” Kwa pande wa Mwenyekiti wa Bodi Mej Generali mst M.J  Isamuhyo alishukuru Wizara kwa kuiamini STAMICO na kumhakikishia kufanya kazi hii kwa weledi mkubwa na kuteleza maagizo yote yaliyotuleta kwa STAMICO. 

Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa SMC Dkt. Venance Mwasse na Mkurugezi Mtendaji wa GGM Bw. Richard Jordinson waliweza kutiliana sahihi na mbele ya Viongozi wengine wa kitaifa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2