TAMWA :RUSHWA YA NGONO TATIZO KWA WANAWAKE WANAOHITAJI NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA VYAMA VYA SIASA | Tarimo Blog

Afisa habari,Sera na Uchechemzi  kutoka Taasisi ya TAMWA Florence Majani akizungumza na waandishi wa habari kwenye mafunzo ya siku moja yanayolenga masuala ya Ushiriki wa Wanawake katika siasa yaliyofanyika Jijini Dodoma leo. Picha zote /habari na Vero Ignatus
Muwezeshaji wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na TAMWA, Wakili Mary Mwita akizungumza na juu ya masuala yanayolenga Ushiriki wa Wanawake katika siasa.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Arusha walioshiriki mafunzo yaliyoandaliwa na TAMWA juu ya Ushiriki wa Wanawake katika siasa yaliyofanyika Jijini Dodoma leo.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini kile kinachoendelea katika mafunzo .



Na.Vero Ignatus.

Vyama vya siasa vimetajwa kuwa chanzo kushindwa kupitisha wanawake kugombea nafasi za uongozi ndani ya vyama huku changamoto kubwa ikiwa ni rushwa ya ngono  kwa wanawake pamoja na udhalilishaji.


Hayo yamesemwa na Afisa habari kutoka Tamwa Florence Majani katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dodoma na Arusha,ambapo alisema baadhi ya wanawake wamekuwa hawana nafasi kwenye siasa na katika ngazi za maamuzi.


Alisema zipo changamoto mbalimbali katika ushiriki wa wanawake katika siasa kwani shida kubwa ipo kwenye vyama vya sisasa,ukiangalia zile kamati zilizopo ndani ya vyama ZEC na NEC hata wakiambiwa wawapeleke  wawakilishi vyama hivyo haviwapeleki wanawake kushindania nafasi za uongozi.


Amesema yapo mambo mengi yanayojitokeza katika kushindwa kwa wanawake kwenye uchaguzi zikiwemo gharama za uchaguzi,mfumo dume unaosisitiza uongozi wa kaya tangia awali,vitendo vya udhalilishaji katika uchaguzi,mfumo mzima wa uchaguzi


Akizungumza muwezeshaji wa mafunzo hayo Wakili Mary Mwita aliweza kutaja ana za udhalilishaji wa kijinsia kuwa ni pamoja na Shambulio la mwili (mfano kuigwa,kusukumwa),kulazimishwa mapenzi bila ridhaa ya mtu mwenyewe(Rushwa ya Ngono)Udhalilishaji wa kisaikolojia (ambapo udhalilishaji huu unatumika zaidi wakati wa uchaguzi)Udhalilishaji wa kiuchumi.


 Aidha aliweza kusema kuwa usawa katika uchaguzi umeainisha mapengo ya jinsia katika sheria tano kwa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia kwamba ni pamoja na kutokubaguliwa kwa njia yeyote ile kwenye mchakato wa uchaguzi ,haki ya kupiga kura ,kuteuliwa ,haki ya kufikia na kutumia rasilimali nza uchaguzi,kuhabarishwa na kusikilizwa,haki ya kuchaguliwa.


Aliwataka waandishi wa habari kutoa taarifa kuhusu manyanyaso juu ya wanawake sambamba na kujielimisha kuhusu masuala ya jinsia na kuzifahamu sheria zinasemaje kuhusiana na maswala ya jinsia,pamoja na kuchambua masuala ya jinsia katika jamii.


Tamko la Kimataifa kuhusu haki za Binadamu la mwaka 1948 ambalo lilibainishwa msingi wa kutokubaguliwa kifungu cha (2)kinakariri kila binadamu ana haki sawa na uhuru bila kubaguliwa kwa misingi ya rangi utaifa jinsi lugha na itikadi za kisiasa

Aidha mkataba wa Kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake 1979 unasisitiza kwamba ubaguzi dhidi ya wanawake ni ukiukwaji wa haki zao za msingi hususani haki ya kuheshimu utu wao na haki zao za msingi.

Ngazi ya kanda maridhiano ya mkataba mwaka 2000 iliingizwa na kubainishwa misingi ya usawa wa jinsia katika kifungu cha 4(1)katika makubaliano yaliyofanyika Lome mwaka 2000

Tamko la shirika la maendeleo kusini mwa Afrika SADC(2005)liliweka kiwango cha jinsia chini ya uwakilishi wawanawake katika kuwa asilimia 30%na baadae kupandisha hadi kufikia 5O%.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2