UBOVU WA MAGARI UNAVYOCHANGIA AJALI ZA BARABARANI | Tarimo Blog



Na.Vero Ignatus


Inasemekana asilimia kubwa ya madereva wanendesha magari yakiwa na mapungufu ,kwaajili ya kulinda vibarua vyao ,na mwisho wa siku safari ambayo walitegemea kwenda hawafiki wanainaishia njiani kwa gari kupata ajali na kusababisha ulemavu au vifo


Baadhi ya Madereva wanalalamika na kuona  kwamba wanaonewa, kuadhibiwa kwa kushindwa kutengeneza magari, ambapo baadhi wamesikika wakisema kuwa wamiliki wa magari ndiyo wanapaswa kuadhibiwa, kutokana na wengine wao kuwa wagumu kutoa pesa za matengenezo, pale dereva anapompelekea taarifa ya uharibifu wa mfumo mmojawapo katika gari.

Jacob Mwanga ni dereva anafanya shughuli zake mkoa wa Arusha,anasema kinachofanya madereva wengi kukamtwa linapotokea tatizo kwenye gari, ni kwamba matajiri wanakuwa ni wagumu kutoa fedha pale gari linapopata hitilafu,anasema wengi wao wanawaambia maderewa pigapiga kazi ukirudi tutarekebisha mwisho wa siku linatokea tatizo la gari kuharibika au kusababisha ajali na dereva anaingia kwenye matatizo.

Anasema madereva wengi ni waoga kuacha gari endapo itakuwa na tatizo, anaona akiacha gari labda inatatizo la breki kwamba atapewa dereva mwingine.Na ndivyo ilivyo tajiri anakwambia kama huwezi mwachie mwingine aendeshe kwahiyo kutokana na njaa zetu dereva utaona anakomaa hivyohivyo mwisho wa siku anapata ajali hata kupelekea yeye mwenyewe kupoteza maisha 

Alitoa rai yake kwa wamiliki wa vyombo hivyo vya moto kuvifanyia ukarabati mara kwa mara, ili kuepusha ajali zitokanazo na ubovu wa magari,ambapo amewataka madereva wenzake kupunguza njaa kwani imekuwa ikiwaingiza kwenye matatizo mara kwa mara .

Afande Athilio Choga kutoka Ofisi ya Afande RTO Arusha Dawati la Elimu amasema kuwa, Kifungu cha 39 cha sheria ya usalama barabarani sura (168)  iliyofanyiwa marekebisho ya mwisho mwaka ( 2002)inakataza chombo chochote cha moto kisichokuwa katika hali nzuri ya kutumika barabarani kisitumike, hivyo kifungu hicho kinataja mifumo ya tairi ya gari  kwamba lazima iwe katika ubora na uwezo wa kufanya kazi vizuri ili kisiweze kuleta hatari ,kwa anayendesha chombo hicho pamoja na mtumiaji mwingine wa barabara.

 Sheria inawataka wamiliki wote wa vyombo vya moto, kuhakikisha kwamba vyombo hivyo vipo katika hali nzuri ndipo akabidhiwe dereva,wakati huohuo dereva anatakiwa kuhakikisha chombo hicho kipo katika hali nzuri ndipo aanze safari,chombo kikiwa kibovu,kinamapungufu dereva hutakiwi kukiendesha,hiyo ni amri ya kisheria ni lazima ifuatwe.Anasema Afande Athilio 

Anaendelea kusema kifungu hicho kinataja mifumo ya injini,breki,gia boksi ,bodi,chesesi ,umeme,kwamba lazima vyote viwe katika mfumo wa kufanya kazi vizuri ndipo chombo cha moto kiweze kutumika barabarani ,aidha kifungu hicho cha 39(1)ndico kinachotoa maelekezo hayo,ila kifungu kidogo cha (2 )kinamkataza mmiliki wa chombo chochote kile cha moto ambacho hakipo katika hali ya ubora kutokuruhusu chombo hicho kitumike barabarani

''Wewe unayemiliki gari kama gari lako ni bovu sheria inakukataza kumruhusu dereva kuliendesha hilo gari,lakini inakataza hata dereva kama gari ni bovu kuendesgha hilo gari kwahiyo wote kwa pamoja ni lazima tushirikiane mmiliki wa gari,dereva pale gari linapokuwa na matatizo ambapo dereva amelibaini asisite kumueleza mmilikiwa gari''alisema Afande Athilio

 Kwa upande wa mmiliki wa gari anatakiwa  kuelewa pale wanapoelezwa tatizo la gari  lake  anapaswa kumsikiliza dereva ili waweze kufanya marekebisho kwenye  hayo  matatizo ili yasiweze kuleta madhara,na  ikitokea mmiliki hamuamini dereva wake badala yake anaweza akamtumia fundi wake wa siku zote kwaajili ya kukagua gari hilo kabla ya kuanza safari na kuhakikisha mifumo yote inafanya kazi sawasawa ili uhakika wa safari uwepo.Alishauri Afande Athilio

''Gari unapolitengeneza likawa katika mfumo mzuri unategemea makosa ya kibinadamu tu ndiyo yasababishe ajali ,haitakiwi gari kusababisha  ajali kutokana na ubovu wake,ajali inapotokea hata mmiliki wa gari wanapata hasara, kwasababu gari litaanguka na litaharibika hata kama unakuwa na bima kuna muda mwingi unapotea kwa shauri kuendelea mahakamani,gari linakuwa kwenye matengenezo,unakuta umepoteza kipindi kirefu bila kufanya biashara hata mzigo wa mteja ulioupakia unakuwa haujafika kwa muda muafaka na unakuwa umeharibika kwenye eneo la ajali ''Anasema

Kwa upande wake Muongoza  watalii Jijini Arusha John Msabi alisema kwa upande wao magari ya kubeba wageni ,ni lazima yafanyiwe ukarabati wa kina na uangalifu mara zote ili kuepusha usumbufu wanapokuwa na wageni, kwani gari linapoharibika linaleta usumbufu kwa wageni  na kumpotezea muda kwani wengi wote  wanakwenda na ratiba ,pia ni aibu siyo kwa kampuni peke yake bali hata Taifa kwa ujumla

Msabi alitoa wito kwa wajasiliamali na wenye makampuni binafsi  ya kukodisha magari ya kubeba watalii,kuyafanyia ukarabati magari yao kabla ya kuyatoa kwaajili ya kuanza safari ,na kuwataka kufahamu kuwa biashara ni ushindani ,hivyo magari yao yakiwa mabovu watakosa soko.

Siku moja nikiwa safarini gari yangu iliharibuka na nilikuwa na wageni,niliona nyuso zao zilivyobadilika na wakaanza kusemezana wao kwa wao,nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kuwa chombo kinaimarika na kuomba radhi kwa wageni wangu na tuliendelea na safari, ila mgeni mmoja alisikika akisema Why Msabi!niliomba radhi tena tukaendelea na safari yetu.

Japokuwa gari inaweza kuharibika popote ila siyo kwa kukusudia unaweza ukawa umefanya ukarabati na ukaguzi wa chombo lakini kwa bahati mbaya tatizo likajitokeza ghafla hiyo inakuwa ni nje ya uwezo alisema John Msabi.  

Faustin Matina Mkuu wa Chuo cha Wide Institute of Driving anasema ubovu wa magari unachangia kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani :Mfano dereva hata kama amesoma kiasi gani na barabara ni nzuri,lakini kama gari ni bovu halina viakisi mwanga na limeharibika barabarani ni rahisi sana kuweza kusababisha ajali 

Anasema ili kupunguza ajali za barabarani nchini Tanzania madereva wanatakiwa kukagua magari na  kuyafanyia matengenezo mara zote kabla ya tatizo halijawa kubwa,kwani faida mojawapo  ni kuepusha ajali zinazotokea barabarani kutokana na ubovu wa magari ,ambapo madereva wakizingatia linakuwa na faida siyo tu kuepusha ajali bali litasabababisha uchumi wa nchi na wa mtu binafsi kuendelea kuwa imara 

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO,Ajali za barabarani humuua  mtu mmoja kila baada ya sekunde 24 ,huku vifo milioni 1.35 vinavuosababishwa na ajali za barabarani vikiripotiwa kila mwaka kote duniani

Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom alisema ajali zinaweza kuzuilika iwapo mikakati muafaka itawekwa ,kwani vifo hivyo ni malipo yasiyo kubalika kwa watembeaji ,hivyo  ni jukumu la serikali ya nchi na washirika kuchukua hatua madhubuti ya kuteteleza mikakati ya kuhakikisha zinakwisha.

 Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Utafiti kutoka (RSA)  Augustus Fungo alieleza Ubovu wa gari huonekana sio kosa la dereva bali la mmiliki aliyeshindwa kulitengeneza gari lake. Na baadhi ya madereva huona kama wanaonewa kuadhibiwa kwa gari bovu,alieleza kuwa dereva anaadhibiwa siyo kwa kushindwa kutengeneza gari bali kwakukubali kuendesha gari bovu.

Fungo alieleza kuendesha gari bovu barabarani kif.39(5)kuwa ni kosa la dereva bila kupepesa macho hapo sheria inasema( any person who uses on a road a motor vehicle or trailer in contravention of the provision of subsection (1),2 or 3 shall be guilty of an offence)hivyo kwa nayekutwa na askari barabarani akiendesha gari ni dereva na ndiyo anaadhibiwa kwa kosa la ubovu wa chombo husika.

''Unachooadhibiwa sio kwa Unaadhibiwa sio kwa kushindwa kutengeneza gari bali kwa kukubali kuendesha gari bovu barabarani kinyume na kifungu cha 39(1) cha sheria ya usalama barabarani''anasema Fungo

Kuendesha gari bovu barabarani (Kif.39(5)anaeleza hilo ni kosa la dereva bila kupepesa macho,hapo sheria inasema, alieleza kushindwa kulifanyia gari matengenezo kifungu cha sheria 39(6)(b)hilo ni kosa la mmiliki au Ofisa,msimamizi wa gari lakini pia linaweza kuwa kosa la dereva kwani kifungu hicho kinatumia maneno (causes or permits)yaani kwa sababu ya kuruhusu gari kutumika ila dereva kwasababu zake mwenyewe akawa amesababisha gari kutumika kwa kuliendesha.

Aidha kuruhusu gari bovu kuendeshwa barabarani (Kif. 39(6)(a)alisema kosa la mmiliki au msimamizi wa gari,pia linaweza kuwa kosa la dereva, kwani kifungu hichi kinatumia maneno (causes or permits) yaani kusababisha au kuruhusu kwa hiyo inawezekana mmiliki asiwe ameruhusu gari kutumika, ila dereva kwa sababu zake mwenyewe akawa amesababisha gari kutumika kwa kuliendesha.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2