WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA LUDEWA 26 WAJITOKEZA ,25 WAREJESHA FOMU | Tarimo Blog


Na Shukrani Kawogo, Njombe

Ikiwa ni siku ya mwisho ya uchukuaji na urudishaji fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Ludewa Mkoani Njombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limekamilika likiwa na wagombe waliochukua fomu hizo 26 na waliorudisha 25 huku mmoja akijitoa katika kinyang’anyiro hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa chama hicho wilayani Ludewa amesema mgombea aliyejitoa ni Christopher Magogo ambaye ni mhadhiri wa Chuo cha Kodi kilichopo jijini Dar es salaam

Alisema kuwa mgombea huyo amejitoa kwa sababu za msingi kwake ambapo amedai kuwa ameamua kujitoa kutokana na kuwa yeye ni mtumishi wa umma na ameona wamejitokeza wagombea wengi sana hivyo ameamua kuwaachia ili waendelee na mchakato na atakayepatikana anaamini kuwa ataleta maendeleo katika jimbo hilo.

Aliongeza kuwa zoezi hilo limeisha salama katika ngazi zote za kata na wilaya ambapo mpaka wanakamilisha zoezi hilo hawajapokea malalamiko yoyote .

Aidha waliokamilisha zoezi hilo la uchukuajo fomu ni Dk. Saimoni Ngatunga pamoja na Augustino Mwinuka ambao walijaza na kurudisha na kufikisha idadi ya wagombea 25.

Na waliorudisha fomu hizo kwa siku ya mwisho ni Dk. Joseph Kamonga, Dk. Suzan Kolimba, Dk. Luka Mkonongwa, Mwl. Fikiri Mgina, Dk. Benda Mwang’onde , James Mkinga, Andru Kuyeyana, Captain Jacob Mpangala na Gerecius Lugome.

Waliorudisha siku zilizopita ni Dk. Primus Nkwera, Kamisha Crodwick Mtweve, Deogratius Nchimbi, Goodluck Mgaya, Barnaba Mhagama, Eng. Alfales Cengula, Dk. Evaristo Mtitu, Baraka Lucas, Mwl. Renatus Njelekela, Dk. Philipo Philikunjombe, Mwl. Herman Yanga, Deo Ngalawa, Dk. Neema Mturo, na Evaristo Mtitu.

Zoezi hilo la uchukuaji fomu limefungwa rasmi leona kuanza mchakato wa kumpata mgombea mmoja atakayekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka huu na kuhusisha vyama mbalimbali vya siasa.
 Mtia nia Captain Jacob Mpangala akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Bakari Mfaume
 Aliyekuwa mbunge viti maalum Dk. Suzan Kolimba akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Bakari Mfaume.

 Mtia nia Andru Kuyeyana, akikabidhi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Bakari Mfaume
 Mtia nia Dk. Joseph Kamonga akitoka katika ofisi ya katibu wa CCM Wilayani Ludewa, baada ya kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Ludewa
 Mtia nia Dk. Joseph Kamonga, akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Bakari Mfaume
 Mtia nia Augustino Mwinuka akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Bakari Mfaume
 Mtia nia Dk. Simon Ngatunga  akirudisha fomu ya kuomba ridhaa kugombea Jimbo la Ludewa kwa Katibu wa CCM Bakari Mfaume
 Mtia nia James Mkinga akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Ludewa kwa katibu wa CCM Bakari Mfaume
 Mtia nia Mwl. Fikiri Mgina akirudisha fomu ya kuomba ridhaa kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Ludewa kwa katubu wa CCM Bakari Mfaume
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2