ASKOFU MAMEO AKEMEA RUSHWA, MATUSI KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI | Tarimo Blog

 WITO umetolewa kwa wanasiasa wote nchini kufanya siasa za kistaraabu na kuepuka rushwa na matusi  katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwenzi Octoba mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Morogoro, Jacob Mameo, wakati wa ibada ya ufunguzi wa nyumba ya mchungaji wa kanisa hilo, Usharika wa Lungo, Mvomero mkoani Morogoro juzi.

 Akizungumza katika ibada hiyo Askofu Mameo aliwataka wanasiasa na mashabiki wa siasa kote nchini kuitunza amani ya nchi kwa kuepuka vurugu, matusi na rushwa nyakati hizi za kampeni.

“Tunawaomba wanasiasa wafanye kampeni zao kistaarabu,waseme sera zao na waache kutukana maana matusi na vurugu sio sera, waseme kile wanachotaka kuwafanyia watanzania. Alisema Askofu Mameo.

 Askofu Mameo aliongeza kusema kuwa kwa miaka mingi nchi yetu imekuwa kisiwa cha amani na hivyo tunapaswa kuendelea kuitunza amani hiyo kwa kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.

 Akizungumzia kuhusu Rushwa, Askofu Mameo alisema kuwa wanasiasa waepuke kutoa rushwa kwa kuwa rushwa hupofusha macho na huondoa uwezo wa kufikiri vema. Kiongozi akiwapa rushwa watu ili wamchague huwafanya watu hao kuchagua pasipo umakini. Alisema kuwa rushwa ni adui wa haki. Kuchagua au kuchaguliwa kwa misingi ya rushwa huwaondolea watu haki ya kupata kiongozi bora.

“Wanasiasa ambao huendekeza rushwa, acheni kutoa rushwa kwa lengo la kushawishi kuchaguliwa. Wanaotoa na kupokea rushwa wanapaswa kutubu kwa kuwa rushwa ni dhambi kubwa ambayo inapaswa kuepukwa kwa kila namna.” Alisema Askofu Mameo.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2