Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAFANYABIASHARA wameaswa kutumia huduma za kiteknolojia zinazotolewa na benki ya Letshego katika kufanya manunuzi na malipo ili kujihakikishia usalama wa fedha zao.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki ya
Letshego Tanzania, Solomon Haule wakati wa uzinduzi wa duka mtandaoni
(App) itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kufanya miamala na
kununua bidhaa mbalimbali kwa haraka.
Haule alibainisha kuwa wafanyabiashara wanapaswa kujilinda zaidi dhidi
ya wizi ambao unaweza kufanyika iwapo kama wakiwa wanatumia fedha
taslim kufanya malipo au manunuzi.
Alisema Teknolojia ya malipo kama hiyo App ya benki, inawahakikishia
wateja usalama zaidi wa fedha zao ambapo mteja anaingia moja kwa moja
kwenye akaunti yake ya benki na kufanya miamala kwa haraka.
Alisema benki hiyo katika utoaji wa huduma zake nchini imeshuhudia
wateja wakipanda kutoka wafanyabiashara wadogo, wa kati hadi kuwa
wakubwa ambapo kutokana na mafanikio hayo imeona kuna haja ya
kuanzisha huduma itakayowezesha wateja kunufaika zaidi.
Alisema,”wateja wetu wakiwemo wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwawatanufaika zaidi na uduma hii kwa kuwa tofauti na huduma nyingine ambazo mteja anapaswa na fedha kwenye akaunti yake ya simu, sisi anakuwa na uwezo wa kuingia kwenye akaunti yake ya benki kwetu moja kwa moja.”
Alisema katika kuhakikisha wafanyabishara wanaendelea benki hiyo
imewawezesha wateja kuomba mikopo kwa njia ya mtandao ambapo mteja
anajaza fomu ya kuomba mkopo anaotaka.
Alisema ndani ya siku 14 maombi yao yatakuwa yameshatekelezwa huku
maofisa wa benki watakuwa na jukumu la kuwafuatilia wateja ambao
watakuwa wakihitaji msaada zaidi.
Benki hiyo yenye makao yake makuu jijini Gaborone nchii Botswana
inafanya kazi nchi 11 huku kwa hapa nchini ina matawi katika mikoa ya
Arusha, Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga na Makambako mkoani
Njombe.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa benki ya Letshego Tanzania, Solomon Haule akizungumza na waandishi habari kuhusiana na matumizi ya teknolojia ya upatikanaji wa huduma kwa kutumia App ya Simu ,jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Benki ya Letshego Zuwena Mohamed 'Shilole' akizungumza namna ya huduma ya App katika simu ilivyomsaidia katika kupata huduma kwa haraka katika benki hiyo.
Watendaji wa benki ya Letshego wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Benki hiyo Zuwena Mohamed 'Shilole' jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment