DKT LWOGA: WANAFUNZI VYUO VIKUU ITUMIENI MAKUMBUSHO YA TAIFA | Tarimo Blog

Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga (katikati), Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure (Wapili kulia), Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa wanafunzi wa Chuo hicho kwenye uzinduzi wa Museum University Hub.
Kulia ni Mtaalam wa Makumbusho ya Taifa Bi Magreth Kigadia, akielezea shughuli za Makumbusho ya Taifa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kushoto mwanzo ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga kwenye uzinduzi wa Museum University Hub.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga, Maafisa wa Makumbusho ya Taifa, Wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Uongozi wa wanafunzi wa Chuo hicho wakiwa tayari kukata keki baada ya uzinduzi wa Museum University Hub.

Na Sixmund Begashe 
WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu nchini wametakiwa kujiunga na umoja kati ya Makumbusho ya Taifa na Vyuo Vikuu ili wapate fursa ya kujifunza kwa matendo namna ya uhifadhi, na kuendeleza Urithi wa kiutamaduni na wa Asilia.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga ambaye pia ndei aliekuwa Mgeni Rasmi katika uzindi uzinduzi wa Umoja huo ujulikanao kama Museum University Hub uliofanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es Salaam. 

“Hii Hub tuliyoizindua leo imeanzia Chuo kikuu cha Dar es Salaam, ni matarajio yetu vyuo vikuu vingine vinavyo fundisha masomo ya Urithi ,Akiolojia, Historia na Utalii vitajiunga ili kutoa fursa kwa wanafunzi katika vyuo hivyo kukutana na wataalam wa Makumbusho ya Taifa ili waweze kushiriki shughuli za Uhifadhi na kuendeleza Mali kale”. Alisema Dkt Lwoga

Nae Mkufunzi Mwandamizi katika fani ya Akiolojia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Egidius Ichumbaki, ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha mashirikiano hayo ambayo yatawapatia wanavyuo wigo mpana wa uwelewa juu ya shughuli nzima za uhifadhi na kuendeleza urithi wa Asili na ule wa Kiutamaduni nchini.

“Kupitia mashirikiano haya Wanafunzi watapata fursa ya kujifunza mambo mbali mbali kupitia wataalam wa Makumbusho ya Taifa lakini pia watapata kushiriki katika shughuli mbali mbali za kimakumbusho, mashauri, Utamaduni, michezo pamoja na mambo mengineyo” Aliongeza Dkt Ichumbaki.

Akielezea uzinduzi wa “Museum University Hub” hiyo Afisa Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Bi Annamery Bagenyi amesema kuwa wametoa nafasi kwa wanafunzi walioudhuria uzindizi huo kutazama onesho maalum lenye kuonesha shughuli mbali mbali za Makumbusho ya Taifa, kujadiliana na wataalam wa Makumbusho hiyo ili waweze kuona fursa za ajira baada ya kumaliza masomo yao.

Licha ya kuushukuru uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha umoja huo, Mratibu wa uzinduzi huo kwa upande wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo hicho Bi Zuhura Mtenguzi amesema wataitumia fusra hiyo kikamilifu ili iweze kusaidia kutimiza malengo yao ya kuwa mahiri katika fani ya uhifadhi na kuendeleza Urithi wa Utamaduni na Mambo kale.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2