Mmoja wa viongozi wa madhebu ya Shia ambae pia ni kiongozi Mkuu wa Chuo cha Dini ya Kiislam kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam, Sheikh. Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari katika maandamano ya amani ya kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain
Sehemu ya waandamanaji wa madhehebu ya Shia wakiwa katika maandamano ya amani ya kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain.
Sehemu ya waandamanaji wa madhehebu ya Shia wakiwa katika maandamano ya amani ya kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain
Wiki moja baada Jumuiya ya Khoja ShiaIthnasheri kupitia programu yake ya “Hussain Blood Drive” kufanikisha zoezi la uchangiaji damu kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama na Hospitali ya Ebrahim Haji, jumuiya hiyo kwa kushirikiana na madhebu yote ya Shia imefanya maandamano ya amani katika kukumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad, (SAAW), Imam Hussain. Maandamano hayo ni muendelezo wa kuadhimisha mwezi mtukufu wa Muharram sambamba na kumbumbuku ya kifo cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain.
Akizungumza katika zoezi hilo, mmoja wa viongozi wa madhebu ya Shia ambae pia ni kiongozi Mkuu wa Chuo cha Dini ya Kiislam kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam, Sheikh. Hemed Jalala alisema “Matembezi haya ya amani ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha cha mjukuu wa Mtume Muhammed (SAWW), Imam Hussain ambae aliuawa zaidi ya miaka 1300 iliyopita huku akiamini katika uhuru na mshikamano ambao hata sisi leo tunauhitaji kwa ajili ya maendeleo na mafanikio ya nchi yetu”.
Sheikh Jalala amesema pamoja na uhuru na mshikamano, Imam Hussain aliamini katika kutunza amani na utulivu jambo ambalo Watanzania wanalihitaji sana hususan kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kubaki kuwa kisiwa cha amani na utulivu. “Lengo la kutoka kwa matembezi haya kwa ajili ya Imam Hussain (as) ni kutaka kupaza sauti kwamba amani, utulivu na upendo ni mambo muhimu ambayo yanapaswa kuenziwa na kutazamwa kwa umakini” alisema Sheikh Jalala.
Maandamano hayo yamefanyika kukumbuka siku ya Ashura ambayo ni siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharram. Zaidi ya Miaka 1300 iliopita, Katika siku hii ya Ashura mjukuu wa Mtume yaani Imam Hussain (as) aliuawa katika tambarare za mji wa Karbala, Iraq. Siku hii huadhimishwa kila mwaka, ili kutunza thamani ya mafundisho ya Imam Hussain (as) ambae alisimamia katika kuamrisha mema na kukataza mabaya. “Amr bil Marouf na Nahy anil Munkar”
Pamoja na maandamano hayo, Jumuiya ya Khoja Shia Ithnasheri imekua ikifanya matukio yanayolenga kusaidia jamii kumuenzi mjukuu huyo wa Mtume. Mambo hayo ni pamoja na zoezi la kuchangia damu huku pia ikiratajia kufanya zoezi la kuendesha uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wenye uhitaji bila malipo yoyote.
Kwa maelezo zaidi:
Tovuti
|
https://bit.ly/32FFE5A
|
|
|
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment