Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli Mwezeshaji wa Jamii kata ya Busangwa, Mary Solo (kulia).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Organization of People Empowerment (OPE) limekabidhi baiskeli tano kwa wawezeshaji ngazi ya jamii kata ya Busangwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ili kusaidia kuifikia jamii kutoa elimu ya masuala ya ulinzi wa mtoto,mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akizungumza leo Ijumaa Agosti 28,2020 Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya amesema shirika hilo wawezeshaji ngazi ya jamii watatumia baiskeli hizo kuifikia jamii katika kutoa elimu ya masuala ya ulinzi wa mtoto,uwezeshaji wananchi kiuchumi na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
“Shirika la OPE tunatekeleza mradi wa Kutokomeza mimba na ndoa za utotoni katika kata ya Busangwa wilayani Kishapu kwa ufadhili wa shirika la Fire Light,hivyo baiskeli hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa wawezeshaji ngazi ya jamii kuifikia jamii”,amesema Kasya.
Ameeleza kuwa shirika la OPE limekuwa likitoa elimu ya wanawake kujitambua na kutambua haki zao ili wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji waweze kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kupata msaada.
“Kazi yetu ni kuijengea uwezo jamii hususani wanawake na watoto wajitambue na kutambua haki zao ili wanapokutana na vitendo vya ukatili waweze kutoa taarifa ili hatua zaidi zichukuliwe”,ameongeza Masya.
Katika hatua nyingine, Kasya amesema suala la ulinzi wa mtoto ni jukumu la kila mmoja katika jamii hivyo jamii inatakiwa kulinda watoto na kuacha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Jamii kata ya Busangwa, Mary Solo amelishukuru shirika la OPE kwa kuwapatia baiskeli ambazo zitawasaidia kuyafikia makundi mbalimbali ya watu katika jamii wakiwemo wanawake,wanaume na watoto kuhamasisha watokomeze mimba na ndoa za utotoni.
Naye Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwanima kata ya Busangwa Maneno Mahenge amesema sasa ataweza kuyafikia maeneo mengi zaidi katika kijiji hicho ili kuwahamasisha kulinda watoto na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya (katikati) akizungumza leo Ijumaa Agosti 28,2020 wakati akikabidhi baiskeli tano kwa wawezeshaji ngazi ya jamii kutoka kata ya Busangwa wilayani Kishapu. Kulia ni Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwanima kata ya Busangwa Maneno Mahenge, na kushoto ni Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwajiningu kata ya Busangwa Evanjelina Jumbe .
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa baiskeli zilizotolewa na Shirika la OPE kwa ajili ya wawezeshaji ngazi ya jamii kata ya Busangwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kusaidia mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwanima kata ya Busangwa Maneno Mahenge (kulia).
Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwajipugila kata ya Busangwa Agustino Ngakayu (kulia).
Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwajiningu kata ya Busangwa Evanjelina Jumbe (kulia).
Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akimkabidhi baiskeli Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Busangwa kata ya Busangwa Challya Gayuka (kulia).
Mwezeshaji wa jamii kijiji cha Mwanima kata ya Busangwa Maneno Mahenge akilishukuru shirika la OPE kwa kuwapatia baiskeli.
Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akipiga picha ya pamoja na wawezeshaji ngazi ya jamii kata ya Busangwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Afisa wa Miradi wa Shirika la OPE, Joseph Kasya akipiga picha ya pamoja na wawezeshaji ngazi ya jamii kata ya Busangwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment