Serikali yaahidi milioni 200 kujenga madarasa DIT Myunga | Tarimo Blog

Na Mwandishi Wetu, Momba (Songwe)
SERIKALI kupitia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo imeahidi kutoa sh milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa madarasa matano katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kampasi ya Myunga ikiyoko Wilaya ya mkoani Songwe.

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Dk Akwilapo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa bwalo la chakula lililojengwa kwa fedha zilizotolewa na serikali kupitia wizara hiyo.

"Nilikua naongea na mkuu wa Taasisi hapa kwamba nikiwapa milioni 200 so mtajenga madarasa matano ili Hawa wanafunzi wasirundikane kwenye darasa moja," alisema Dk Akwilapo.

Ahadi hiyo ilikuja kufuatia ombi la wanafunzi la kuomba serikali kuboresha niundombinu ya kujifunzia ikiwa ni pamoja na madarasa, uwanja wa michezo na vifaa vya michezo pamoja na gari la kwaajili ya kwenda kwenye mafunzo viwandani.

Dk Akwilapo alisema anaamini kwa fedha hizo DIT itajenga madarasa mazuri yenye ubora unaofaa kwa kutumia wataalamu wa ndani wa Taasisi hiyo.

Aidha katika tukio hilo, Dk Akwilapo aliahidi pia kumlipia ada mwanafunzi wa pili TEHAMA, Nozen Mkubwa ambaye alikuwa na changamoto ya ulipaji ada Jambo ambalo lilikuwa likimkwamisha katika masomo yake.

Akizungumzia ujenzi wa bwalo hilo, aliipongeza Taasisi hiyo kwa usimamizi mzuri wa rasilimali fedha uliofanikisha kukamilika ujenzi huo kwa asilimia 100.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam, Profesa Preksedis Ndomba alishukuru serikali na Katibu Mkuu huyo kwa msaada ambao umekuwa ukitolewa na serikali kupitia wizara hiyo na kuahidi kuendelea kusimamia vema miradi inawekezwa na serikali katika Taasisi.

Mkurugenzi wa Kampasi ya DIT Myunga, Dk Frank Lujaji alishukuru kwa msaada wa kijana Nozen kulipiwa ada ambapo alitoa wito pia kwa Taasisi nyingine kusaidia vijana wenye changamoto za kupata ada kwani wengi Wana uwezo wa kimasomo pamoja na nia ya kusoma.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2