Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Agosti 26, 2020 ametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kupitia msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kupita bila kupingwa katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kongwa.
Akitangaza matokeo hayo kwenye ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dkt. Omary Nkullo amesema Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Ndugai ndiye pekee aliyekidhi vigezo vilivyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kumfanya kupita bila kupingwa.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa amepita bila kupingwa, Mheshimiwa Ndugai amesema anawashukuru wana CCM, viongozi na wanachama kwa ujumla kwa heshima waliyompatia na kumwezesha kupita bila kupingwa.
“Nahaidi kila haina ya ushirikiano kwa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na kuhakikisha uchaguzi wa Jimbo la Kongwa unaenda vizuri, kwa amani na salama”alisema Spika Ndugai
Pia, Mheshimiwa Ndugai ameahidi kuwa ataendelea kuwa mtumishi wa wanaKongwa na kuwa mwakilishi wao katika maeneo mbalimbali.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment